Judith Ferdinand,Mwanza
MWANAUME Pastory Majura (52) mkazi Kijiji cha Nyamanga wilayani Ukerewe jijini Mwanza anashikiliwa na Polisi akituhumiwa kwa kosa la mauaji ya mkewe, Anusiata James (52).
Chanzo cha mauaji huyo ni mume kumfumania mke wake nyumbani kwake akiwa na mwanaume mwingine ambaye alikimbia baada ya fumanizi hilo.
Akizungumza Jijini Mwanza jana Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza ACP.Muliro Jumanne, amesema tukio hilo lilitokea Aprili 10, mwaka huu saa 10 alfajiri katika kijiji cha Nyamanga Kata ya Ukara baada ya mtuhumiwa kumpiga mke wake na kitu kizito kichwani baada ya fumanizi.
Amesema mume wa marehemu ambaye kwa sasa ni mtuhumiwa mara baada ya kufanya shambulio hilo alijichoma na kitu chenye ncha kali tumboni na kupata maumivu makali. Amesema mwanaume huyo amelazwa Hospitali ya Wilaya ya Ukerewe akiendelea kupata matibabu.
Pata habari kamili kwenye Gazeti la Majira…
More Stories
Premier Bet yamtangaza mshindi mkubwa
Dkt. Kazungu atembelea miradi ya umeme Dar es Salaam
MSF ilivyojidhatiti kusaidia serikali katika utoaji wa huduma za afya