January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Atletico Madrid yakataa ofa ya Liverpool kwa Niguez

MADRID, Uhispania

KLABU ya Atletico Madrid, imekataa ofa ya Liverpool pauni milioni 35 kwa ajili ya kumyakuwa kiungo wao Saul Niguez ili aweze kuitumikia timu hiyo msimu ujao.

Wiki iliyopita kocha wa Liverpool Jurgen Klopp alikuwa amemlenga Sauli kama mbadala wa Georginio Wijnaldum, ambaye aliondoka kwa uhamisho wa bure kujiunga na Paris Saint-Germain, huku wakiweka mezani pesa hiyo kumpata mchezaji huyo.

Hata hivyo, Liverpool haina wasiwasi sana juu ya fedha wanazotaka Atletico ili waweze kumtoa Niguez ambaye inasemakana thamani ya mchezaji huyo karibu pauni milioni 45.

Ikiwa Liverpool itaongeza zabuni, Atletico iko tayari kukubali na kumruhusu Sauli matakwa yake ya kuondoka, lich y Brcelona nayo kuwania saini ya mchezaji huyo.

Barcelona wamekuwa wakimwinda Saulo kwa miaka na wanaamini msimu huu wa joto ndio nafasi yao nzuri ya kumsaini. Walipendekeza makubaliano ya kubadilishana ambayo yangemleta Sauli Camp Nou badala ya Antoine Griezmann anayependwa na Atletico.