Na Joyce Kasiki, Tanga
MBUNIFU Luqman Luvanda ametambulisha mashine ya Atlas, inayozalisha gesi kwa kutumia maji, akisema teknolojia hiyo inalenga kusaidia matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini Tanzania.
Akizungumza katika banda la Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwenye maadhimisho ya Kitaifa ya Elimu,ujuzi na Ubunifu Luvanda amesema, mashine hiyo huzalisha gesi inapohitajika na inaweza kutumika kwenye majiko mbalimbali bila kusababisha moshi, masizi au uchafuzi wa mazingira.
Amesema teknolojia hiyo inaendana na azma ya Tanzania ya kuhamia kwenye nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034.
Mbunifu huyo amesema Atlas imetengenezwa nchini na aliweza kushiriki maonesho hayo kupitia msaada wa Coasttech, baada ya kushinda mashindano ya ubunifu.
Amesema wanatarajia kuanza kuipeleka teknolojia hiyo sokoni mwezi Desemba, huku wakilenga kuendelea kuboresha mashine hiyo ili iwe rahisi kubebeka na kutumika katika maeneo mbalimbali.

More Stories
Mbunifu wa dawa salama apunguza uharibifu wa mayai
Tulia Trust kuja kivingine,tamasha ngoma za asili
Rais Samia kuandika historia mpya leo uzinduzi wa JNHPP