November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Atlas Schools Marathon sasa ni Oktoba 18

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

MBIO za Atlas ‘Atlas School Marathon’ ambazo hufanyika kila ifikapo Oktoba 14 ikiwa pia ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Nyerere ‘Nyerere Day’ zimesogezwa mbele hadi Oktoba 18.

Taarifa iliyotolewa na mmiliki wa shule hiyo, Sylivanus Rugambwa ilisema kuwa,
Bodi ya wakurugenzi na uongozi wa shule hiyo umeamua kusogeza mbele mbio hizo pamoja na mahafali ya wahitimu wa kidato cha Nne na Darasa la Saba kwa campusi zote tunasogeza mbele shughuli za mahafali na mbio za Marathon (ATLAS DAY) ambazo.

Amesema, waliona si busara kufanya shughuli hizo ikiwa Rais wa Jamhuri (CCM), Dkt. John Magufuli atakuwa na ziara ya mikutano ya hadhara Wilaya ya Kinondoni ambapo atakutana na wananchi.

“Bodi ya Wakurugenzi tuliona siyo heshima kuwa na matukio mengine yenye kuvuta hadhira ya watu katika eneo ambalo ziara ya mheshimiwa Rais inafanyika na ndio maana baada ya kuvishirikisha vyomb mbalimbali Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Baraza la Michezo Tanzania, Riadha Taifa na Riadha Mkoa, Bodi iliona ni vema kusogeza mbele shughuli za mbio na mahafali mpaka Jumapili ya Oktoba 18,” amesema Rugambwa.

Licha ya kuahirishwa kwa mbio hizo kwa siku kadhaa, Rugambwa amesema kuwa wanaendelea na maandalizi ya mbio hizo na wakiwa kama wazalendo wataendelea kumuenzi Hayati Baba wa Taifa Mwl Julius K. Nyerere.

Katika mashindano hayo kwa upande wa kilometa 21 washindi wa kwanza kwa upande wa wanawake na wanaume atazawadiwa kiashi cha Sh. 400,000, Sh. 250,000 kwa washindi wa pili, Sh. 200,000 kwa washindi wa tatu, Sh. 150,000 kwa washindi wa nne, watakaoshika nafasi ya tano watapewa Sh 100,000 huku wanataoshika nafasi sita hadi ya 10 wakipewa Sh. 50,000 kila mmoja.

Kwa upande wa mbio za kilometa 10, watakaoshika nafasi ya kwanza kwa upande wa wanawake na wanaume watapata Sh. 300,000, Sh 200,000 kwa washindi wa pili, Sh, 150,000 kwa watakaoshika nafasi ya tatu, Sh. 100,000 kwa watakaopata nafasi ya nne na Sh. 30,000 kwa watakaoshika nafasi ya tano hadi 10.

Kwenye mbio za kilometa tano zawadi zitakuwa Sh. 100,000 kwa washindi wa kwanza wanawake na wanaume, Sh. 75,000 kwa msindi wa pili, msindi wa tatu ataondoka na Sh. 50,000 huku nafasi ya nne hadi ya 10 wakipewa Sh. 20,000.