December 28, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Athari za nchi kutoridhia mkataba wa CFA kwageuka kikwazo

Na Penina Malundo, Kigali

BAADHI ya nchi kutoridhia utiaji saini Mkataba wa Pamoja wa
Bonde la Mto  Nile (Cooperative Frame Work Agreement-CFA) chini ya usimamizi wa Mradi wa Bonde la Mto Nile (NELSAP),kunazinyima nchi hizo fursa ya kunufaika na matokeo ya miradi kwa wananchi wake.

Miongoni mwa mataifa ambayo hadi sasa hayajatia saini,mkataba huo ni Kenya na Burundi, huku nchi nyingine nne za nne za kikanda ambazo ni Tanzania,Ethiopia,Uganda na Rwanda, zenyewe zimetia saini mkataba huo wa pamoja katika kutekeleza miradi yao.

Akizungumza mjini Kigali nchini Rwanda na waandishi wa habari, Meneja Mradi wa Kanda kutoka wa mradi wa NELSAP yaani Nile Equatorial Lakes Subsidiary Action Program Coordination Unit, (NELSAP -CU) Mhandisi ,Dkt. Issac Alukwe amesema kuna umuhimu wa
kuwepo kwa ufumbuzi wa haraka katika nchi ambazo hazijatia saini, ili kuwezesha utekelezaji wa miradi ya maendeleo kufanyika kwa lengo la kubadilisha maisha ya watu katika mataifa husika.

Mhandisi Daktari Alukwe amesema hatua ya baadhi ya nchi kutotia saini kunasababisha nchi hizo zilizo ndani ya makubaliano ya kutumia Bonda la Mto Nile  kuchelewa kunufaika na faida zitokanazo na miradi mbalimbali ya kikanda chini ya usimamizi ya mradi wa bonde hilo, ikiwemo miradi ya Nishati,usimamizi wa maji na miradi mingine ya kijamii.

Amesisitiza kuwa taifa la Kenya hawajatia saini mkataba huo, lakini wameendelea kuwafuatilia na kuwakumbusha kila wakati ili waweze kufanya hivyo.

”Tunajua kwamba nchi ya Misri kuna mambo fulani hawajakubaliana bado,  hususani katika upande wa ugawaji wa maji sababu iliyowaafanya kuendelea kusita kutia saini,japo kuwa majadiliano yanaendelea,”amesema

Hata hivyo akizungumzia nchi ya Burundi , Dkt Alukwe amesema kutokana na majadiliano wanaweza kutia saini mkataba huu wa CFA muda wowote.

Eng,Issack amesema kuwa athari zimekuwa nyingi kwa taasisi ya bonde la mto Nile yaani, Nile Basin Initiative (NELSAP ), liloundwa na nchi hizo kwa lengo la kusimamia maendeleo katika bonde la mto Nile.

“Tunategemea wafadhili katika kutafuta hela na wafadhili  wanaangalia muundo wa maamuzi ya kisheria kwani hadi sasa baadhi ya nchi hazijaweka saini na kusababisha NBI  kutokuwa na mkataba wa pamoja katika nchi hizo hivyo kusababisha utafutaji wa fedha kuwa mgumu kupatikana kwaajili ya maendeleo ya bonde hilo,” amesema.

Akitolea mfano kwa mwaka 2023, amesema Umoja wa Ulaya (EU) walitaka kutoa kiasi fedha, Euro Milioni 10 kwa NBI, badala yake waliamua kuahirisha kwa muda kutokana na sababu ya zilizopo katika nchi hizo mbili.

Kinachoendelea kwa sasa kwa mjibu wa Injinia Alukwe mazungumzo na umoja wa Ulaya, EU ili kuweza kupata fedha hizo,kwani EU bado wanaonekana kufurahia kazi yao NELSAP na viwango vya utekelezaji kazi hizo vinaheshimika.