May 15, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

ATE wazindua Tuzo ya Mwajiri bora wa mwaka 2022

Na Jackline Martin, TimesMajira Online

Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) wamezindua rasmi Tuzo ya Mwajiri Bora wa mwaka 2022 ambapo lengo la Tuzo hiyo ni kutambua na kutoa Tuzo kwa Waajiri wenye misingi Bora ya usimamizi wa nguvu kazi na rasilimali watu pamoja na kutambua Waajiri wanaofanya biashara kwa kuzingatia sheria na taratibu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Tuzo hizo, Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa ATE Suzanne Ndomba alisema kutokana na marejeo na Uboreshaji wa Mchakato wa Utoaji wa Tuzo hizo, Tuzo zitakuwa na vipengele 14, kutoka vipengele 27 vya awali;

“Kipengele Cha (Managing During Crisis)-Namna ambavyo makampuni yanakabiliana na majanga yanayotokea katika maeneo ya kazi, (Climate change/Environmental management)-Mabadiliko ya Tabia ya nchi), (Gender Equality and Equity-(Haki na usawa wa kijinsia) na (Compliance with Regulatory Requirements)- ukidhi wa matakwa ya kisheria”

Ndomba alisema mbali na mabadiliko hayo ambayo lengo ni kuziboresha Tuzo hizo na kuongeza ushindani miongoni mwa washiriki, wataendelea kuwa na Tuzo ya mshindi wa Jumla, Tuzo kulingana na ukubwa wa Taasisi /Kampuni, Waajiri Bora katika sekta binafsi, sekta ya Umma pamoja na mashirika ya ndani ya nchi , Tuzo ya Mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO) na Tuzo ya Local Content (Maudhui ya ndani).

Aidha Ndomba alisema Tuzo hizo zimeendelea kuhamasisha Waajiri kuendelea kurekebisha na kufanya vizuri zaidi katika maeneo mbalimbali pa kazi;

“Tangu kuanzishwa kwa Tuzi ya Mwajiri Bora wa mwaka , imeendelea kuhamasisha Waajiri kuendelea kurekebisha na kufanya vizuri zaidi katika maeneo mbalimbali mahala pa kazi pamoja na kuzingatia sheria na kanuni zilizowekwa ili kuongeza tija mahala pa kazi, kufanya biashara ki mantiki na kupunguza migogoro mahala pa kazi “

Mbali na hayo Ndomba alisema kitabu kilichoboreshwa Cha mwongozo wa msingi muhimu ya kusimamia Rasilimali watu ya Tuzo ya Mwajiri Bora wa mwaka kitakuwa tayari hivi karibuni.

Ikumbukwe kuwa Tuzo ya Mwajiri Bora wa mwaka (EYA) ni zoezi lililoanzishwa na kuendeshwa kila mwaka na Chama Cha Waajiri Tanzania tangu mwaka 2005, ambapo inalenga kuwatambua wanachama wao waliofanya vizuri katika kuweka mikakati Bora yenye kutathimini usimamizi wa rasilimali watu na shughuli za kibiashara