Na Jackline Martin, TimesMajira Online
Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) wamezindua rasmi mchakato wa kutafuta Mwajiri bora wa Mwaka 2023 lengo ni kuwatambua waajiri wanaofanya vizuri katika kuweka mikakati bora yenye kuthamini na kuzingatia usimamizi wa rasilimali watu ili kuongeza tija katika biashara.
Hayo ameyasema Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa ATE, Suzanne Ndomba wakati akizungumza na waandishi wa Habari katika uzinduzi huo ambapo alisema
Tukio la tuzo hizo litafanyika mapema mwezi Disemba mwaka huu.
“Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka imeendelea kuwa tukio muhimu kwa Waajiri wote nchini linalotambulika katika ngazi ya kitaifa ambapo kwa miaka kadhaa sasa tuzo hizo zimehamasisha Waajiri kuweka sera bora za ajira na usimamizi wa rasilimali watu, kuchochea na kuongeza tija, mahusiano bora Mahala pa kazi, utii wa sheria na ushindani kibiashara .”
Aidha Ndomba amevitaja Vipengele vya Utoaji wa Tuzo hizo kwa mwaka huu 2023.
“Ubora katika Usimamizi wa Rasilimali Watu,
Tuzo ya Utofautishwaji na Ushirikishwaji,
Masuala ya Utawala na Uongozi, Ukuzaji wa Vipaji, Corporate Social Responsibility (CSR),
lakini pia Ushirikishwaji wa Mwajiriwa”
“Uwajibikaji katika mwenendo wa biashara na utendaji unaokidhi,
Mafunzo ya Ujuzi wa kazi na Uanagenzi, Maudhui ya Ndani, Ubora, Uzalishaji na Ubunifu, Mbadiliko ya Tabia Nchi”
Aidha Ndomba ameendelea kuvitaja vipengele hivyo ikiwemo Namna ambavyo makampuni yanakabiliana na Majanga yanayotokea katika Maeneo ya Kazi mfano Janga la UVIKO 19, Usawa wa Kijinsia na Usawa katika Maeneo ya Kazi lakini pia Kampuni Inayofuata Miongozo na Matakwa ya Kisheria.
Sambamba na vipengele hivyo, Ndomba amesema pia wataendelea kuwa na Tuzo ya Mshindi wa Jumla, Tuzo zinazotolewa kulingana na ukubwa kwa Kampuni, Tuzo ya Waajiri bora katika sekta binafsi, Tuzo ya Waajiri katika Sekta ya Umma, Tuzo za mashirika yasiyo ya kiserikali lakini pia
Tuzo ya Mwajiri Bora Mzawa.
Ndomba amewaomba waajiri wote wajitokeze kwa wingi kushiriki katika mchakato huo muhimu wa kumtafuta Mwajiri Bora wa Mwaka ambaye atatangazwa rasmi katika tukio kubwa la utoaji wa Tuzo hizo kwani tuzo za mwaka huu 2023 zitakuwa na mabadiliko makubwa ukilinganisha na mwaka uliopita.
More Stories
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu