Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online
Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) inapenda kuwajulisha Wafanyakazi Wastaafu wa ATCL
na Wanachama wa Ushirika wa Akiba na Mikopo (Wanahewa SACCOS) kuwa Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imelipa madeni yaliyotokana na malimbikizo ya michango.
Madeni hayo ni michango ambayo haikuwasilishwa kwenye uliokuwa Mfuko wa Pensheni wa
PPF katika kipindi cha kuanzia mwezi Mei, 2008 hadi Oktoba, 2016 pamoja na ile ya
Wanahewa SACCOS kwa vipindi mbalimbali kabla ya mwezi Oktoba, 2016.
Utaratibu wa malipo hayo kwa wanufaika kwa sasa unaratibiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii
kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) pamoja na Wanahewa SACCOS ili kuhakikisha kila
mwanachama anapata stahiki yake kwa mujibu wa Sheria.
Kwa taarifa zaidi kuhusu malipo tajwa tafadhali wasiliana na PSSSF pamoja na uongozi wa
Wanahewa SACCOS.
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua