December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

AT amshukuru Harmonize

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

MSANII wa muziki wa staili ya miduara kutoka Zanzibar

AT, amemshukuru msanii wa muziki wa Bongo fleva na Bosi

wa Kondegang Rajabu Abdul maarufu kama ‘Harmonize’ kwa

kumfanya aonekani kwenye ramani ya mziki kwa sasa.

Akitoa shukrani hizo, AT amesema Harmonize ni kijana

pekee mwenye uthubutu wa kumsaidia kila mtu, kwani

amekuwa naye karibu na kufanya naye mambo makubwa.

“Nimekuwa nikifanya kazi kwa Kuzingatia Ukubwa wako na

Heshima ya Watu wetu wote. Nichukue nafasi hii

kukushukuru wewe Harmonize na kila shabiki wako na

Uwongozi Mzima Kwa kufanya Leo AT azungumzike,

atizamike Upya, pamoja na kuwashukuru kwa Dhati Media’s

Zote kwa kila sekta na Fans wangu na Wasanii wenzangu

wote wanaonipenda na wasionipenda mimi niseme Shukran

sana sana Mubarikiwe.

Naomba nitoe ahadi ya kufanya Kazi nzuri zaidi na kwa

uadilifu. Wazanzibar naomba niwaambie tu. Huyu Kijana

ni ndugu yetu, anaroho ya kipekee tokea nimekuwa nae

karibu na Kuna Makubwa kwa Bara na Visiwani kwetu. Kaa

tayari kupata kitu kizuri,” amesema AT.