Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Maridhiano mkoa wa Dodoma Askofu Dkt.Evance Chande amesema ukatili unaoendelea katika mikoa mbalimbali hapa nchini kutoka na maasi kuongezeka na jamii kutokuwa na hofu ya Mungu huku akiiasa jamii kumrudia Mungu.
Dkt.Evance ameyasema hayo kufuatia vcitendo vya ukatili vinaendelea ambavyo vimekuwa vikitokea katika mikoa mbalimbali hapa nchini ukiwemo mkoa wa Dodoma.
“Hapa kwenye kumuasi Mungu ndio msingi mbaya wa matukio na vitendo vya ukatili unapioanzia ,maana kama watu wanamcha Mungu haiwezekani kufanya matukio kama hayo.”amesema Dkt.Evance na kuongeza kuwa
“Watu hawapaswi kabisa kujenga misingi hiyo ya kuuana kwani hakuna sababu yoyote ya kufanya hivyo…,tujenge tabia ya kusameheana badala ya kuweka madukuduku moyoni ambayo baadaye hupelekea kulipiza kisasi.”
Kufuatia hali hiyo,kiongozi huyo ameitaka jamii kutubu na kumsujudia Mwenyezi Mungu ili irudi kwenye misingi ya upendo,amani na utulivu na kluachana na vitendo vya ukatili.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Zabibu Mtoro amesema,chanzo cha matukio hayo ya ukatili ni pamoja na chuki .
Ameiasa Serikali kuliangalia suala hilo na kuona namna ya kukomesha vitendo hivyo huku akiwaasa viongozi wa dini kukemea na kuhubiri amani,upendo na mshikamano kila wakati katika nyumba zao za Ibada bila kujali itikadi zao za dini.
Akihubiri katika ibada ya kawaida katika Kanisa la Asemblies Of God Ipagala mwishoni mwa wiki ,Mwinjilisti wa Kanisa la EAGT Manchali wilayani Chamwino mkoa wa Dodoma William Njanii amewaasa wazazi kuwajenga misingi ya kuwaonya watoto wao pindi wanapoona wanafanya matukuio yasiyompendeza Mungu.
Aidha ameiasa jamii kubadilika huku akiwaasa watumishi wa Mungu kuendelea kuihubiria jamii maneno ya Mungu bila kuchoka ili kuinusuru jamii dhidi ya vitendo vya ukatili.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba