Na Moses Ng’wat, Timesmajira Online,Mbozi.
JESHI la Polisi Mkoa wa Songwe limewaonya askari wake wenye ndoa kuacha tabia ya kuwapeleka watoto kulelewa kwa bibi na babu kwa kufanya hivyo husababisha malalamiko huku wengi wao kukosa huduma muhimu na uangalizi wa karibu zaidi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Theopista Mallya, alitoa onyo hilo wakati akito nasaha zake alipohudhuria ibada ya misa ya ndoa ya Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Antony Sabasaba, ambaye ni Msaidizi wa Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilaya ya Momba.
Tukio hilo la Sakramenti ya ndoa takatifu lilifanyika katika kanisa la Katoliki Jimbo Kuu la Mbeya, Parokia ya Mtakatifu Patrick Mjini Vwawa, wilayani Mbozi.
“Kuna ‘statement’ nimesikia umesema hapo padre kuwa wanandoa wawe tayari kupokea watoto na kuwalea, huo ni wosia muhimu sana kwani tunapata kesi nyingi sana za askari kupeleka watoto kwa wazazi wao na kuwatelekeza bila matunzo,”amesema Mallya na kuongea kuwa
” Yaani mzazi amekuzaa, amekulea na kukusomesha hadi umepata kazi kisha unafunga ndoa na unazaa halafu unampelekea mtoto akulele,hapa hilo halikubaliki na mimi nitalisimamia na kuchukua hatua,”.
Pia, amewataka askari kuwa mfano bora kwenye jamii kwa kuimarisha malezi ya familia zao ili kuwa na familia zenye kuchukia uharifu.
Aidha, Kamanda Mallya ameihasa jamaii kuwa na utaratibu wa kuwa karibu na familia zao ili kuimarisha malezi ya watoto hali ambayo itasaidia kupunguza vitendo vya ukatili kwa watoto na kuwaepusha kujiingiza kwenye uharifu.
More Stories
Kilo 673.2,dawa za kulevya zakamatwa Bahari ya Hindi
Watoto wenye uhitaji wapatiwa vifaa vya shule
Wananchi Kisondela waishukuru serikali ujenzi shule ya ufundi ya Amali