Judith Ferdinand,Timesmajira Online,Mwanza
Askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza Kitengo cha Usalama Barabarani Wilaya ya Nyamagana WP 3984 Sajenti Stella Alfonce(49), amepoteza maisha akiwa kazini mara baada ya kugongwa na gari la shule ya msingi Nyamuge.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Wilbrod Mutafungwa ameeleza kuwa ajali hiyo imetokea leo Novemba Mosi majira ya saa 12 na dakika 45 asubuhi barabara ya Mwanza/Musoma eneo la Nyamhongolo wilayani Ilemela.
Ambapo gari yenye namba za usajili T.964 BRJ aina ya Mitsubishi Rosa mali ya shule ya msingi Nyamuge iliyokuwa ikiendeshwa na dereva Philipo Mhina(52),mkazi wa Nyasaka ambaye alisimamishwa na Stella aliyekuwa na wenzake katika kituo hicho cha ukaguzi wa magari.
Mutafungwa ameeleza kuwa baada ya kukaguliwa gari hiyo ilikutwa na kosa ndipo dereva alipoambiwa arudishe gari nyuma kwa ajili ya usalama wa watumiaji wengine wa barabara.
Ameeleza kuwa wakati akirudi nyuma alimgonga Askari huyo kwa nyuma na kusababisha kifo chake hivyo jeshi hilo linamshikilia dereva huyo.
Hata hivyo ameeleza kuwa jeshi hilo linaendelea kutoa wito kwa madereva na wananchi kuendelea kuchukua tahadhari,kufuata sheria za usalama barabarani na kujali watumiaji wengine wa barabara ili kuepusha madhara yanayoweza kuepukika yatokanayo na ajali za barabarani.
More Stories
Kyobya: Watakaohusika kudhoofisha jitihada za Serikali,Pori la Akiba Kilombero kushughulikiwa
Wenje:Tuwanadi wagombea bila kuchafuana
Mtoto darasa la tatu adaiwa kujinyonga kwa kukosa nguo ya sikukuu