Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Askari wa Jeshi la Polisi Mkoani Mtwara, WP Husna Juma Baraka, ameibuka mshindi wa pikipiki katika droo ya saba ya Kampeni ya NMB MastaBata ‘Kote Kote’ inayoendeshwa na Benki ya NMB, ambayo hadi sasa imeshatoa zawadi zenye thamani ya Sh. Milioni 138 kati ya zaidi ya Sh. Mil. 300 zinazoshindaniwa.
NMB MastaBata Kote Kote ni kampeni inayohamasisha matumizi ya kadi za NMB Mastercard na Lipa Mkononi (kuscan QR), badala ya pesa taslimu, ambako droo hiyo ilisimamiwa na Ofisa wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Irene Kawili na kufanyika katika Tawi la Bank House.
Akizungumza kabla ya droo hiyo, iliyoambatana na makabidhiano ya pikipiki kwa mshindi wa droo ya sita, Charles Shemsanga, Kaimu Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Faraja Ng’ingo, alisema licha ya kuchagiza matumizi ya kadi, lakini pia wanaitumia MastaBata Kote Kote kuwazawadia wateja wao msimu huu wa sikukuu.
Aliwataka wateja wa NMB kuendelea kufanya miamala mbalimbali kupitia NMB mastercard na Lipa mkononi( mastercard QR) kufanya malipo kwenye migahawa, supermarket, vituo vya mafuta na hata sehemu za starehe, ili kujiongezea nafasi kubwa ya kushinda zawadi kemkem za kampeni hiyo.
Kupitia kampeni hii, Blue Santa wa MastaBata anawazawadia washindi 75 kila wiki kiasi cha Sh. 100,000 kila mmoja, huku mmoja akitwaa pikipiki, pikipiki mbili kwa washindi wawili wa kila mwezi – sambamba na washindi 49 wa pesa taslimu Sh. Mil. 1 kila mmoja kwa droo za mwezi na grand finale, safari ya Dubai kwa siku 4.
More Stories
Elon Musk : Bill Gates atafilisika endapo…
CRDB yazindua matawi Majimoto, Ilula kuwahudumia wananchi
Lina PG Tour yafufua gofu Moshi