January 25, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

ASAP Rocky: Nimebarikiwa na Mungu kuwa na Rihanna

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

MSANII wa rap nchini Marekani A$AP Rocky, amefunguka kuhusu mahusiano yake na mpenzi wake Rihanna na kusema anajiona mtu mwenye bahari ya kubarikiwa na Mwenyezi Mungu kuwa na mpenzi kama Rihanna.

Akizungumzia hilo, A$AP Rocky amesema Rihanna amekuwa msaada mkubwa sana kwenye maisha yake kwani alikuwa bega kwa bega wakati anatambulisha makala yake ya Stockholm Syndrome iliyohusu stori yake ya kukamatwa na kutiwa jela nchini Sweden mwaka 2019.

“Nilitaka tu kusimulia stori yangu bila kuonekana na lalamika au nimeonewa”. Kwenye makala hiyo A$AP Rocky anasimulia tukio la mwaka 2019 jinsi timu yake ilivyogombana na vijana wawili huko nchini Sweden na kujikuta akiwekwa jela bila dhamana sababu alikuwa mgeni.