Na Esther Macha, Timesmajira Online, Mbeya
Imeelezwa kuwa kupitia Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW),imesaidia Mkoa wa Mbeya kufikisha asilimia 87.6 ya watu wazima wanaojua kusoma na kuandika huku Serikali ikiombwa kuwekea mkazo katika Wilaya ya Mbarali na Chunya zilizopo mkoani humo.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima ( TEWW), Profesa ,Philipo Sanga, kwenye ufunguzi wa mafunzo ya maofisa usafirishaji na mama lishe juu ya elimu ya ujasiriamali, usalama barabarani, afya na mazingira.

Amesema mbali na Mkoa wa Mbeya kufanya vizuri bado kuna asilimia 12 hawajui kusoma na kuandika huku Mkoa huo ukiendelea kushika nafasi ya tano katika mpango wa serikali wa kuangalia Mikoa ambayo kuna baadhi ya watu wazima hawajui kusoma, kuhesabu na kuandika.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Mkuu wa wilaya ya Mbeya,Solomon Itunda, amesema katika mpango wa mikoa ambayo baadhi ya watu wake hawajui kusoma, kuhebu kuandika wao wapo vizuri.
‘ Sisi tuna asilimia 12 ya watu wazima ambao hawajui kusoma na kuandika,bado tupo vizuri , lakini maeneo mengine hususani kwenye elimu ya msingi na sekondari tumeendelea kufanya vizuri kitaifa kwa kushika nafasi ya pili,”amesema Itunda.
Sanjari na hayo amesema mpango huo wa miaka 50 ya taasisi hiyo kufikia kundi la wasafirishaji na mama lishe kutoa elimu ya matumizi ya usalama barabarani, afya, ujasiriamali na mazingira utakuwa msaada kwa makundi hayo.
Pia amewasisitiza bodaboda kujiepusha na vitendo vya uharifu na kuwataja wanaofanya vitendo hivyo.Kwani wapo baadhi wanaohusuka na matukio ya ukatili na uharifu hivyo amewataka kuwa sehemu ya kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Hata hivyo kiongozi wa bodaboda Mkoa wa Mbeya,Aliko Fwanda, amewataka wasafirishaji kuacha vitendo viovu ambavyo baadhi yao wamekuwa wakiharibu sifa ya kundi hilo ,
“

I
“
.

More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako