January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Arsenal yakamilisha usajili wa Martin Odegaard

LONDON, England

KLABU ya Arsenal imekamilisha usajili wa kudumu wa

mchezaji Martin Odegaard kutoka Real Madrid ambaye

alikuwa akiitumikia timu hiyo kwa mkopo.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Norway, ambaye

anajiunga na Arsenal kwa kitita cha pauni milioni 30

pamoja na bonasi yenye jumla ya thamani ya karibu

pauni milioni 4.

Odegaard, mwenye umri wa miaka 22, alikuwa London

Jumatano akifanya vipimo vya afya baada ya vilabu

hivyo viwili kufikia makubaliano.

Mchezaji huyo alitumia nusu ya pili ya msimu uliopita

kwa mkopo ndani ya kikosi cha The Gunners baada ya

kushindwa kupata nafasi kwenye kikosi cha Real Madrid

chini ya kocha Zinedine Zidane.

Alicheza mara 20 kwenye mashindano yote, na moja ya

magoli yake mawili ni kwenye ushindi wa Derby ya

Kaskazini mwa London dhidi ya Tottenham mnamo Machi.