UONGOZI wa Hoteli ya APC wameiomba serikali kuongeza siku na muda wa maonesho ya 48 ya biashara ya kimataifa sabasaba kwani bado watu wanauhutaji mkubwa wa huduma zao na wao kupata fursa ya kuendelea kujitangaza.
Hayo yamesemwa leo na Afisa Masoko kutoka APC Hotel Conference Center – Happy Sanga katika maonesho hayo ambayo yanatarajiwa kufunguliwa kesho na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Jamhuri ya Msumbiji Filipe Nyusi.
Amesema lengo lao ni kuvutia wawekezaji na Watalii wengi nchini na hivyo kukuza uchumi na pato la Taifa.
“Tunaiomba Serikali kuongeza muda wa maonyesho kutoka saa 12 jioni mpaka saa sita usiku au kuongezaa siku za maonyesho haya kwani bado watu wanahitaji lakini pia sisi pia tuna uhitaji wa kujitangaza na kutumia fursa hii kuendelea kuwatumia watanzania wengi zaidi”
Aidha amesema Mwitikio wa maonesho hayo ya 48 ni mkubwa na kuwasihi wale ambao hawajafika katika Banda lao waweze kufika na kupata huduma zao zilizo bora.
“Mwitikio wa maonesho ya sabasaba ni mkubwa sana na tumepata watu wengi ambao wametembelea Banda letu, niwakaribishe ambao bado hamjafika mje kutembelea Banda letu kwenye jengo la Kilimanjaro Banda namba 22”
“Tunazawadi nyingi ambazo mteja atazipata pale atakapofika katika Banda letu”
Kuhusu Huduma wanazozitoa katika hoteli hiyo ambayo inapatikana maeneo ya Bunju Mtaa wa Misumi, Sanga amesema wanajihusisha na kumbi za mikutano Si chini ya 10 ambayo inachukua kuanzia watu watano hadi elfu moja, inayohusisha mikutano ya ofisi na binafsi ambayo imeambatana na huduma za ya chakula pamoja na maladhi.
Pia amesema Wana huduma ya swimming pool na michezo ya watoto lakini pia viwanja vya michezo kama vile netball , basketball, volleyball na tenes.
More Stories
Mhandisi Samamba awasisitiza maafisa madini kusimamia usalama wa migoni msimu wa mvua
Wapinzani kutimkia CCM ishara ya ushindi Uchaguzi Serikali za Mitaa
Vikundi Ileje vyakabidhiwa mikopo ya asilimia 10, DC Mgomi avipa somo