Judith Ferdinand,TimesMajira Online, Mwanza
Mama wa mtoto Debora Elias mwenye umri wa miaka miwili,kutoka Tarime vijijini mkoani Mara anayesumbuliwa na tatizo la kichwa kikubwa,anaomba msaada kwa watanzania na serikali kwa ujumla kiasi cha laki tatu(300,000),ili mtoto huyo aweze kupata vipimo kabla ya kufanyiwa upasuaji wa kuondoa mpira kichwani(shanti) ambao umeshuka mpaka shingoni.
Akizungumza na majira mama mzazi wa Debora, ameeleza kuwa mtoto wake alitakiwa kufanyiwa vipimo vya CT-Scan Aprili 19, lakini mpaka sasa bado hajafanikiwa kupata kiasi hicho.
Ameeleza kuwa mtoto wake mara ya kwanza alifanyiwa upasuaji kichwani na kuwekewa mpira(shanti), akawekewa mpira baada ya muda ukafeli,akafanyiwa tena upasuaji mara ya pili na kuwekewa mpira wa pili nao ukafeli,watatu pia umefeli sasa anatakiwa kuwekewa mpira kwa mara nyingine.
Mama huyo ameeleza kuwa mpira umeshuka hadi kwenye shingo sasa wanasema hawezi kutolewa mpaka afanyiwe hicho kipimo cha CT-SCAN na vingine kisha ndio watoe mpira huo na kumuwekea mwingine
“Kabla ya kumfanyia upasuaji wa kuondoa mpira huo na kuwekewa mwingine anatakiwa kufanyiwa vipimo ikiwemo cha CT-Scan ambacho gharama yake ni shilingi laki mbili (200,000), kipimo cha damu 41000, kipimo cha figo 7000 pamoja na gharama za dawa baada ya upasuaji,”ameeleza.
Hivyo amewaomba watanzania,wadau na serikali imsaidie mtoto wake ili apate matibabu kwani hana msaada wowote na uwezo wake ni duni ambapo kwa mujibu wa Daktari ni kuwa mpira umeshuka na mtoto huyo kwa sasa ameshindwa kutambaa wakati awali kabla ya mpira kushuka alikuwa ameanza kutambaa.
“Naomba msaada mwanangu apate matibabu sina msaada mme wangu alifariki wakati nikiwa na mimba ya Debora,nahangaika mwenyewe familia imeisha nikataa,hivyo nikija kwenye kituo nakaa mpaka nipate mtu anidhamini tangu mtoto wangubkuwa na tatizo hili siwezi kufanya vibarua nasubilia msaada na hapa nimewaacha watoto wangu wengine watatu wanahangaika wenyewe nyumbani,”ameeleza mama huyo.
Kwa upande wake Ofisa Uhusiano wa Nyumba ya Matumaini, Joanitha Joachim,ambayo ipo kwa ajili ya kuwasaidia watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi, ameeleza kuwa kwa upande wa mama Debora anachangamoto kwa sababu tangu mwanzo alifanyiwa kipimo na kufanyiwa upasuaji lakini Shanti(mpira) ulifeli hivyo mtoto akahitajika kufanyiwa upasuaji mara ya pili.
Ambapo pia alitakiwa kufanyiwa kipimo cha CT-Scan ambapo waliongea na wadau wakamchangia na mtoto alifanyiwa upasuaji na kurejea nyumbani ambapo hali yake ikiendelea vizuri.
“Mara ya tatu sasa karudi ambapo mtoto ana changamoto shanti(mpira) umeshuka ambapo anatakiwa afanye kipimo cha CT-Scan ili waweze kuona mpira ulipo waweze kuutoa na kuwekewa mpira mwingine lakini kwa sasa ana changamoto ya fedha kwa ajili ya vipimo kwani ndugu zake wamemtenga huku mme wake ambaye angemsaidia ameisha fariki hivyo kasimama yeye kama yeye,”ameeleza Joanitha.
Joanitha ameeleza kuwa msaada wanaotoa kituo kwa watoto wenye changamoto hizo ni kutafuta wadau ambao wataweza kuwasaidia kwa ajili ya gharama za vipimo lakini mpaka sasa hawajaweza kupata lakini kama kituo wanampa sehemu ya kulala na chakula maana hawahitaji arudi nyumbani kabla ya kupata matibabu.
Pia kituo hicho kinasaidia watoto hao mpira(Shanti) wa kuwekewa kichwani bure huku huduma ya upasuaji kwa watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano anafanyiwa upasuaji bure lakini kwa upande wa vipimo mzazi ndio anapaswa kugharamia.
“Alipewa wiki mbili ili kufanyiwa upasuaji hivyo alipaswa kufanyiwa Aprili 19, lakini mpaka sasa bado kutokana na kukosekana kwa fedha kwa ajili ya kufanyiwa vipimo kabla ya upasuaji,ikiwa ni pamoja na CT- Scan ambayo ugharimu laki mbili,7000 kwa ajili ya kuangalia figo kama zipo vizuri,41000 kwa ajili ya vipimo vya damu, operesheni bure kituo kinatoa mpira anaowekewa mtoto kichwani kwa ajili ya kushusha maji,”ameeleza Joanitha na kuongeza kuwa
“Nawaomba watanzania wamsaidie mtoto huyu kiasi cha laki tatu kwa sababu hatujui baada ya kufanyiwa upasuaji akiingia wodini kitahitajika kitu gani gharama za kulazwa na dawa zitakuwaje, ili aweze kuwa na furaha kama watoto wengine,”.
Mawasiliano ya kumchangia Debora Elias ni M-Pesa 0742675927 jina linalotoka Regnatha John au unaweza kufika katika kituo hicho Nyumba ya Matumaini (Hope House Nyegezi majengo mapya wilayani Nyamagana mkoani Mwanza)
More Stories
Kiswaga:Magu imepokea bilioni 143, utekelezaji miradi
Zaidi ya milioni 600 kupeleka umeme Kisiwa cha Ijinga
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini