December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Anjella aweka rekodi hmpya

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

MSANII muziki wa Bongo felva na mwandishi wa nyimbo kutoka lebo ya muziki Konde Music Worldwide (KMW) , Anjella amejikusanyia views zaidi ya Milioni 7.97 kwenye mtandao wa YouTube kupitia maudhui ya nyimbo zake zote.

Anjella, alijiunga na mtandao wa YouTube mwezi Oktoba 25, 2020 na amekuwa na wastani wa kutengeneza views zaidi ya milioni 1 kila mwezi kupitia kazi zake mbalimbali ambazo amezipakia kwa takribani kipindi cha miezi 7 na nusu.

Ikumbukwe nyota huyo wa muziki wa kizazi kipya wiki iliyopita alikabidhiwa Plaque (Silver Button Award) na mtandao wa Youtube baada ya kufikisha wafuatiliaji (Subscribers) zaidi ya 100,000.