December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Anelisa, Benpol rasmi wavunja ndoa yao

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

MFANYABIASHARA na Mrembo ambaye Raia wa Kenya Anerlisa Mungai, amethibitisha kuwa tayari amesaini talaka iliyowasilishwa mahakani na aliyekuwa Mume wake msanii wa bongo fleva Bernard Paul Mnyang’nga maarufu kama ‘Benpol’.

Akithibitisha hilo kupitia kwenye Ukurasa wake wa Instagram (Insta-Story) Anerlisa amesema tayari kile kitu ambacho mwenzake alikihitaji mahakamani ameshakitimiza.

Inaripotiwa Shitaka hilo lilifunguliwa katika moja ya mahakama ya mwanzo jijini Dar es salaam huku chanzo kilichopelekea msanii huyo kuchukua maamuzi hayo bado hakijajulikana

Ikumbukwe kuwa ndoa kati ya BenPol na Anerlisa ilifungwa mwishoni mwa mwezi May 2020 katika kanisa katoliki la Mt Gasper Mbezi Beach Dar es salaam.