Na Patrick Mabula, Kahama
SERIKALI ya Mtaa wa Shunu uliopo Halmashauri ya mji wa Kahama imemkamata mwanamke, Janeth Nzemya (39) kwa tuhuma za kumuunguza na kisu cha moto kwenye kiganja cha mkono mwanae wa kuzaa wa kiume mwenye umri wa miaka tisa.
Afisa mtendaji wa mtaa huo,Ignatus Mwacha alisema kuwa, mwanamke huyo walimkamata juzi asubuhi kwa tuhuma za kumuunguza mtoto wake kwa kisu cha moto katika kiganja cha mkono wa kulia na kumjeluhi vibaya.
Mwacha alisema Nzemya walimkamata baada ya kupata taarifa toka kwa wasamaria wema juu ya tukio hilo la mama huyo kuwa amemfanyia ukatili manae wa kiume kwa adhabu ya kumchoma na kisu.
Alisema, baada ya kumkamata mwanamke huyo na kumhoji alikiri kukiweka kisu kwenye moto na kumchoma kwenye kiganja chake cha mkono kwa madai ni mtukutu, mwizi na amekuwa akiwalawiti wadogo zake na watoto wa majirani zake na kuamua ampe adhabu hiyo.
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo,Richard Mwandu alisema, tukio hilo liliwashtua na kuwasikitisha sana kutokana na majelaha ya kuunguzwa na kisu cha moto kwa mtoto huyo kwa madai ni mtukutu.
Naye mama huyo Nzemya alipoulizwa na waandishi wa habari alikiri kutoa adhabu hiyo kwa mwanawe kwa kile alichodai kuwa ni mtukutu, mwizi na amekuwa na tabia ya kuwalawiti watoto wenzake katika mtaa huo na kudokoa vitu vya watu.
Nzemya alisema, mtoto wake amekuwa na kesi nyingi anazozipokea kutoka kwa watu za udokozi na amekuwa akimuonya mara kwa mara na kuamua kumpatia adhabu hiyo.
Alisema, awali mtoto wake alikuwa anaishi na mjomba wake anayeishi jijini Mwanza ambae hakupenda jina lake litajwe ambae aliamua kumrejesha kwake na kila anapofanya kosa anapomuuliza tabia hiyo ameitoa wapi huwa anadai alifundishwa na watoto rafiki zake aliokuwa anaishi nao huko jijini Mwanza.
ìNdugu zagu waandishi wa habari naomba niwaeleze ukweli juu ya mtoto wangu huyu nilishatumia viongozi wa madhebu ya dini wakiwemo wachungaji pamoja na kuwatumia majirani zangu ili ajirekebishe, aache tabia ya kulawawiti wezeka na wizi laki hakuna mabadiliko, ndipo nilipoamua kumpa adhabu hiyo nikiwa na lengo aweze kuacha,”Alisema Nzemya.
Viongozi wa serikali ya mtaa huo wa Shunu walisema, baada ya kupata maelezo ya mama huyo waliamua kumpeleka kituo cha polisi kwenye dawati la jinsia ili sheria ichukue mkondo wake na walikiri kupokea mwananke na kudai hawawezi kueleza lolote kwa kuwa si wasemaji.
More Stories
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa
NLD kipo tayari kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa