January 25, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Amber Lulu: Jamani tuzaeni

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

MSANII wa muziki wa Bongo fleva na Video Queen hapa nchini Amber Lulu, ambaye hivi karibuni amejifungua mtoto wa kike ajulikanaye kama Iam, amewataka wanawake wazae huku wakiwalea watoto wao katika misingi mema.

Akiweka wazi hilo kupitia kwenye Ukurasa wake wa Instagram Amber Lulu amesema, siku zote Watoto anatakiwa kulelewa katika misingi Mema na yenye kumpendeza Mwenyezi Mungu.

“Tuzaeni jamani ila tusisahau kuwalea vizur katika misingi bora na ya kumpendeza mungu. Baby mama Iam Arianna26,” ameandika Amber Lulu kupitia kwenye Ukurasa wake wa Instagram.