Na Bakari Lulela, Timesmajira Online,Dar
Jijini Dar-es-Salaam,licha ya kuwa na upinzani wa maneno na kutupiana vijembe kwa kila mmoja kunadi timu, inayo mpa ulaji.Kampuni ya Rockmax,imewapa ubalozi wasemaji wa timu za mpira wa miguu za Simba SC na Yanga, Ally Kamwe na Ahmed Ally wa bidhaa ya saruji (Cement) ya extra power skimmy putty.
Akizungumza mara baada ya kupata ubalozi huo,Msemaji wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema, kutokana na ushawishi walionao katika jamii,ndiyo sababu ya kampuni ya skim extra power imeamua kuwachagua.
Amesema Kupitia kampuni hiyo inatoa fursa muhimu kwa kijana ambaye amewekeza na kuajiri vijana wengi wa kitanzania.
Msemaji wa Yanga na Balozi wa bidhaa hiyo Ally kamwe amesema,hatua yakuwa Balozi wa bidhaa hiyo wamejiridhisha katika suala la ujenzi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar-es-Salaam Mkurugenzi wa kampuni ya Skimming Putty, Hamoud Shabiby amesema kuwa, makubaliano kati ya mabalozi hao nikutokana na ubora wa wa bidhaa yao inayoongoza Afrika Mashariki.
“Killa mfuko wa extra power skim,utakuwa na coupon ya sh. 2000 itakayomuwezesha mtumiaji kutumia kwenye simu yake kama vocha au salio la M-pesa, Tigo pesa,”amesema Hamoud.
More Stories
Watakaokwamisha mapato Kaliua kukiona cha moto
Dkt.Gwajima aagiza kuundwa kamati za ulinzi wa watoto
Kilo 673.2,dawa za kulevya zakamatwa Bahari ya Hindi