Na Lubango Mleka, Times Majira Online – Tabora.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora limethibitisha kumshikilia Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe kwa tuhuma za kuwachafua viongozi wa Serikali.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao amethibitisha hayo kwa kusema kuwa Kamwe anashikiliwa tokea jana(Aprili 2,2025),baada ya mchezo wao na Tabora United,ambapo amesema wanaendelea na mahojiano juu ya tuhuma hizo na taarifa zaidi zitatolewa baadae.

“Kweli tunamshikilia msemaji wa Yanga Ally Kamwe kwa tuhuma za kuwachafua viongozi wa Serikali ,tulimkamata jana saa saba usiku na tunaendekea kumhoji tutakapo kamilisha mahojiano tutatoa taarifa kamili,”
Ally Kamwe anashikiliwa kwa madai ya moja ya mikutano yake na mashabiki wa Yanga kabla ya mchezo wa jana kati ya Tabora United dhidi ya mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara alimkashifu Mkuu wa Mkoa wa Tabora Paul Chacha.

More Stories
Waziri Mavunde azindua rasmi shughuli za uchimbaji madini Porcupine North -Chunya Mbeya
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Baraza la Taifa la Ujenzi waingia makubaliano ya mashirikiano sekta ya ujenzi
Nderiananga aongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa tatu wa Kimataifa wa watu wenye ulemavu ujerumani