December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Aliyeanguka na kupata ulemavu apatiwa msaada wa kiti mwendo

Na Esther Macha,Timesmajira,Online, Mbeya

NAIBU  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Mbeya Mjini Dkt. Tulia Ackson ametoa msaada wa kiti mwendo pamoja na kifaa cha kufanyia mazoezi kwa Ramadhan Mwanjelile mkazi wa Kata ya Uyole Jijini humo aliyepata ulemavu wa kupooza viungo .

Msaada  huo umetolewa kwa mwananchi huyo baada ya kuanguka miaka minne iliyopita na kupata ulemau wa kudumu .

Akitoa msaada huo wa kiti mwendo Dkt. Tulia amesema kuwa ameguswa na mwananchi huyo kutokana na changamoto kubwa anayopata  baada ya kupata hitilafu ya mwili wake bila kupata mafanikio ya kupona.

“Katika jamii kuna changamoto nyingi sana kama mbunge nimekuwa nikijitahidi kwa kilac namna kusaidia makundi  yenye watu wenye ulemavu maana unajua hujafa hujaumbika huyu mwezetu alizaliwa mzima lakini kwa bahati mbaya amekuja kupata ulemavu huu  baada ya kuanguka na hakupona tena na ndo kawa mlemavu wa kudumu mpaka leo “amesema Dkt. Tulia.

Kwa upande wake ,Ramadhan Mwanjelile mkazi wa Kata ya Uyole ambaye amepata ulemau baada ya kuanguka amesema kitendo alichofanyiwa na Naibu spika hana cha kumlipa zaidi ya kumshukuru kwa alichofanya .

“Binafsi nashindwa niseme nini kwani muda mrefu sasa nilikuwa nimelala kitandani kutokana na tatizo kubwa nililopata la kuanguka limenifanya niwe tegemezi maana siwez fanya chochote,kupitia msaada huu wa kiti mwendo naamini sasa nitaweza hata fanya shughuli ndogondogo za kuniingizia kipato ili kuendesha maisha yangu na familia”amesema Mwanjelile.

Hata hivyo alimshukuru  Mbunge kwa kumjali na kumpatia kiti mwendo ambacho kitamsaidia pia kujisogeza kufanya mazoezi kutokana na kupata shida mrefu pasipokuwa na mazoezi yeyote zaidi ya kulala.

“Huu msaada kwangu ni mkubwa kwani meza ya mazoezi nayo ni msaada mkubwa  kwani familia yangu  isingeweza kumudu kununua vitu hivyo kutokana na hali duni tulinayo ya kimaisha “amesema .

Mmoja wa wanafamilia hao Paulina Mwanjalile amesema  kwamba ndugu yao alikuwa na changamoto kwa muda mrefu hivyo kupitia msaada huo wanaamini kwamba ataweza kufanya mazoezi sasa na kufanya kazi zingine za kumwingizia kipato .

“Unajua aliyoanguka huyu ndugu yetu hatukutegemea kama angeweza kuja kupata ulemavu huu tuliona ni utani lakini miaka inazidi kwenda,tunamshukuru mungu kwa Mbunge wa jimbo la Mbeya kujitokeza kumsaidia kupata kiti mwendo”amesema  Mwanjalile.