December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ali Kiba aitaka jamii kuacha Kilimo cha Whatsapp

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira

MSANII wa muziki wa Bongo na Bosi wa lebo ya KingsKiba hapa nchini, Ali Kiba ametoa ushauri kkuhusu faida ya Kilimo na changamoto zake kwa wadau mbalimbali.

Kupitia mtandao wake wa Twitter Alikiba amewataka watu kuachana na kilimo cha mitandao (Whatsapp) na badala yake kuhakikisha wanafika mashambani ili kujionea hali halisi.

“Nilileta staili za ufanyaji wa muziki kwenye kilimo mwanzoni, niliisoma namba. Kilimo cha ‘Whatsapp’ ni shida,” amesema Ali Kiba

Hivi karibuni nyota huyo wa muziki aliweka wazi kuwa kwa muda sasa amekuwa akijihusisha na shughuli za kilimo na akaahidi kutoa somo kuhusu vitu alivyojifunza kwenye kilimo.