December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

ALAT wampongeza Mhandisi Mahona kwa utendaji kazi

Na Mary Margwe,  TimesMajira Online, Simanjiro

Mjumbe wa Jumuiya za Tawala ya Mitaa Tanzania ( ALAT )  Mkoa wa Manyara na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Mji wa Mbulu  Yefred Myenzi amempongeza Mhandisi wa Ujenzi wa Halmashauri ya wilaya ya  Simanjiro Mkoani humo  Daniel Charles Mahona kwa uwajibikaji wake  katika kusimamia ikamilifu ujenzi wa jengo la Utawala la halmashauri ya wilaya ya simanjiro.

Hayo alizungumza juzi wakati wajumbe wa ALAT Mkoa wa Manyara chini ya mwenyekiti wake Peter Martin Sull, walipofanya ziara yao wilayani Simanjiro ambapo pamoja na mambo mengine kamati hiyo ilifanya kazi ya kukagua miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na ujenzi unaoendelea wa jengo la Utawala la halmashauri hiyo.

Myenzi amempongeza Mhandisi Mahona kwa kile alichodai kuwa kijana huyo amekua akitumia vizuri kipaji chake, taaluma yake kikamilifu katika kusimamia miradi kwa weledi  mkubwa na wa kipekee, ambapo majengo mengi aliyosimamia yako tofauti na majengo mengine Mkoani humo.

Myenzi ambaye kabla ya kuwa halmashauri ya Mji wa Mbulu, alitokea halmashauri ya wilaya ya Simanjiro, alisema bila kuwa na maslahi yoyote ya Mhandisi Mahona, amempongeza kwa juhudi katika utendaji wake wa kazi katika majengo ya Halmashauri hiyo kikamilifu.

“‘Kipekee sana bila kuwa na maslahi yoyote naomba nimpongeze Mhandisi wa Halmashauri ya wilaya hii Mahona, tulianza ujenzi hapa wakati hapakua na Mhandisi kabisa, yaani jitihada niliyofanya ili kuweza kumpata yeye kwa kweli ilikua ni ziada, nadhani katika majengo yote tuliyopitia nadhani mmeona kuna standadi  fulani ya ujenzi ” alisema Myenzi.

” Kipaji chake, utaalam yake lakini pamoja na kusaidiwa na wengine mimi naomba nisifiche hisia zangu, nimpongeze sana mhandisi wa halmashauri ya wilaya hii  kwa utendaji wake wa Kazi, hakika ni mhandisi anayetumia kipaji chake kikamilifu na uadilifu wa hali ya juu sana, pia anamtaka Mkandarasi wa ujenzi wa jengo hilo la Utawala SUMA JKT kuhakikisha wanatumia muda wao vizuri kama walivyoahidi kumaliza ujenzi huo Julai 30, mwaka huu, aliongeza Myenzi

Aidha naye  Kaimu Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Serikali za Mitaa  Mkoani hapa Jackson Kisaka alimtaka Mkandarasi wa mradi huo SUMA JKT kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa halmashauri kuangalia namna ya kuongeza nguvu kazi katika shughuli hiyo ili jengo hilo liweze kwenda haraka, kwa kile alichosema kuwa ni la muda mrefu.

” Jengo liko vizuri ni kweli lakini linakwenda kwa kazi ndogo sana, Kwa hiyo mkandarasi liangalie hili kwa umakini mkubwa, maana linauliziwa uliziwa sana ni la muda mrefu, hata ukienda vikao vingine ,viongozi wanaliulizia sana sana kuwa mbona jengo  ni la muda mrefu ,tatizo ni mini SUMA JKT au wameshindwa? alihoji katibu Tawala hiyo msaidizi sehemu ya Serikali za Mitaa.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa ALAT Mkoa huo na Mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Mbulu Peter Martin Sulle alisema kikubwa alichokiona hapo ni mkandarasi kuweza kuongeza nguvu kazi ili mradi uweze kwenda kwa kazi zaidi.

” Mwisho wa siku kazi hii itatakiwa kuamalizika kwa muda uliokadiriwa, kama alivyosema Afisa Kisaka kwamba shughuli hii ni ya muda mrefu kidogo hata kule halmashauri ya Wilaya ya Mbulu imekuja nyuma yenu, wenzenu wameshaingia mjengoni kitambo sana ninyi hapa bado, haitupi picha nzuri kama Mkoa” alisema Sulle.

Aidha kufuatia hilo Mwenyekiti huyo, aliitaka mkandarasi SUMA JKT kuhakikisha jitihada zinafanyika ili kuendana na muda walioupanga kukamilisha ujenzi huo, kikubwa ni kuongeza nguvu kazi ili shughuli hiyo iweze kukamilika Kwa wakati stahili.

” Chamsingi ni kuongeza nguvu kazi hapa ili shughuli hii ikamilike kwa wakati, serikali iendelee kutupa imani kwa kusimamia mradi kwa weredi lakini kutekeleza kwa wakati na kwa viwango vinavyostahili, kila la heri wanasimanjiro katika utekelezaji wa majukumu yenu, miradi tumeipitia, tumeashauri lakini pia palipostahili kuagiza tumeagiza” aliongeza Mwenyekiti hiyo wa ALAT Mkoa wa Manyara.

Mhandisi wa Ujenzi wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro Daniel Charles Mahona alisema halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro iliingia  mkataka na wakala wa majengo ( TBA ) kwa ajili ya kufanya kazi za kuandaa michoro , kudizaini  jengo na kuwa mshauri wa mradi  kuwa mkataba Na.LGA/06/2026-2017/NS/01,  mkataba huo ulikua ni wa miezi 18 kuanzia agosti 4, 2017 hadi agosti 4, 2019 baadaye ya muda kuisha mkandarasi mshauri aliongezewa muda wamiwzi 12 hadi agosti 4, 2020.

Mhandisi Mahona alisema thamani ya mradi huo ni sh. Bil.5,233,009,800.2, mradi unaotekelezwa na mkandarasi Mjenzi  SUMA JKT kwa mkataba No. LGA/062/2017/2018/W/06 na kusainiwa chini ya usimamizi wa Mkandarasi Mshauri ( TBA ).

” Katika kutekeleza majukumu ya mkataba huo,  mshauri wa mradi  ( TBA ) ameonyesha mapungufu katika kutekeleza majukumu yake ikiwa ni pamoja na kutokaguakazi zilizofanywa namkandarasi kwa wakati, baada ya muda wa mkataba kuisha, Halmashauri ilifikia maamuzi ya kutohuisha mkataba na mkandarasi mshauri , maamuzi hayo yaliambatana na barua kutoka kwa katibu mkuu TAMISEMI yenye kumbukumbu Na.CHB.114/501/01/06 ya Julai 3,2020 ambapo katibu Mkuu  aliiridhia halmashauri kutohuisha mkataba na TBA ” alisema Mahona.

Aidha Mahona alisema barua yenye kumbu Na.HMW/SMJ/U/VOL.lll/46/18 ioiandikwa na Mkoani kwaajili yakumuomba mhandisi wa Mkoa kushirikiana na mhandisi wa wilaya kuendelea kumsimamia mkandarasi ( SUMA JKT) anayejenga hilo la Utawala.

Aidha ujenzi ulianza kwa kufuata taratibu zote za ujenzi ikiwa no pamoja na kutafiti udongo,kunyoosha kwa kutumia ‘total station’ ujenzi wa msingi  ( substructure )  kazi ya zege ( nguzo mlalo,nguzo wima na sakafu – slabs ) ujenzi wa kuta ( Partition walls) , mpaka sasa jengo limekwisha pauliwa na kufunikwa.

” Kazi zinazoendelea  ni kutengeneza sakafu ya kwanza, kuunganisha miundombinu ya Maji safi na Maji taka, kuunganisha mfumo wa umeme, mawasiliano namfumo wa moto, hadi kufikia mwishoni mwa mwezi sita kazi  za kifitisha madirisha na umaliziaji wa sakafu ya kwanza zitakua zimekamilika, ambapo utekelezaji wa kazi zote mwaka septemba 30, 2022 ulifikia asilimia  62 ” alifafanua Mahona.

Akielezea juu ya malipo mbalimbali yaliyokwishalipwa alisema jumla ya sh bil.2,181,239,407.29 Kati ya sh. bil.5,233,099,800.82  ambayo ni jumla kuu ya gharama ya ujenzi huo wa jengo la Utawala, ambapo wamepeleka tena maombi ya fefha hadhina  kwa kutumia hati ya malipo Na.6 yenye thamani ya sh.mil.360,767,106.61 kwa ajili ya malipo kwa Kazi za umaliziaji zinazoendelea.

Akielezea changamoto zilizojitokeza alisema ni pamoja na Mkandarasi  SUMA JKT  kushindwa kukamilisha ujenzi kwa kutumia fedha zake, na  kutegemea malipo ya Mshitiri.

Kufuatia hilo halmashauri ya wilaya ya Simanjiro ilichukua hatua ambapo katika kikao cha mradi  (Site meeting )  kilichofanyika  Machi 9, 2022 kikao kiliazimia kuwa Mkandarasi aongeze mafundi, pili Mkandarasi aliahidi kuleta vifaa eneo la mradi na kuendelea na kazi  ili malipo yaendelee kufanyika.

Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji alimuongezea Mkandarasi  SUMA JKT muda wa mwaka mmoja kuanzia Julai 30, 2021 hadi Julai 30, 2022 ili aweze kukamilisha ujenzi wa jengo hilo.

Mhandisi wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara Daniel Charles Mahona akisoma taarifa ya mradi ya ujenzi wa jengo l Utawala LA halmashauri hiyo, juzi mbele ya kamati ya ALAAT Manyara chininya mwenyekiti wake Peter Martin Sulle ( aliyevaa suti ya bluu  hapo mbele ), (Picha na Mary Margwe)