January 5, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Akamatwa kwa kumuua mke wake kwa fimbo

Na Esther Macha,TimesMajira,Online, Mbeya

MKAZI wa Mswiswi wilayani Mbarali mkoani Mbeya, Samson Kyando (26) anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumuua kwa kumpiga na fimbo sehemu mbali mbali za mwili mke wake, Cecilia Wilson (24) kutokana na ugomvi wa kifamilia uliohusisha marehemu na mtuhumiwa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Ulrich Matei, alisema tukio hilo lilitokea Oktoba 4, mwaka huu saa 2 usiku katika kijiji cha Mswiswi wilayani Mbarali.

Kamanda Matei amesema mtuhumiwa alimshambulia marehemu, Cecilia kwa kumpiga na fimbo na kumsababishia majeraha hali iliyopelekea kukimbizwa hospitali misheni Chimala kwa matibabu.

Aliendelea kudai kuwa Oktoba 6, mwaka huu saa 4.00 usiku, Cecilia alifariki wakati akipatiwa matibabu hospitalini hapo na kwamba inaelezwa kuwa chanzo cha ugomvi huo ni ugomvi wa kifamilia baina ya marehemu na mtuhumiwa.

Kamanda Matei amesema upeleklezi washauri hilo unaendelea na baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.

Matei alitoa wito kwa jamii kuacha tabia yakujichukulia sheria mkononi na badala yake wajenge tabia ya kutafuta suluhu ya migogoro yao kwa kukaa meza moja ya mazungumzo au kushirikisha watu wa karibu ili kupata suluhisho la migogoro yao