March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Airtel yawatembelea Wateja, Mawakala Jijini Dar es Salaam

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online DSM

KATIKA kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja 2025, kampuni ya mawasiliano ya Airtel Tanzania imefanya ziara maalum ya kuwatembelea wateja na mawakala wake katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.

Ziara hiyo, iliyolenga kusikiliza maoni ya wateja, kuonyesha ubunifu wa huduma, na kuthibitisha dhamira ya kampuni kupitia kaulimbiu yake ya “Mteja Kwanza”, ilihusisha timu ya Airtel Tanzania ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji, Charles Kamoto.

Timu hiyo ilitembelea maeneo ya Tandika, Kariakoo, na Mbagala, ambapo walipata fursa ya kuzungumza na wateja na mawakala wa Airtel kuhusu uzoefu wao katika matumizi ya huduma za kampuni hiyo, Mazungumzo hayo yalibainisha jinsi huduma na suluhisho za kidijitali za Airtel zinavyorahisisha maisha ya kila siku na kuongeza urahisi wa mawasiliano kwa Watanzania.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Kamoto amesema:

“Wiki hii tulitaka kutoka ofisini na kwenda moja kwa moja kwa wateja na mawakala wetu. Tulitaka kusikiliza maoni yao, kuelewa changamoto wanazokutana nazo, na kuhakikisha huduma zetu zinaendelea kuboreshwa ili kukidhi mahitaji yao.”

Kupitia juhudi hizo, Airtel Tanzania inaendelea kuthibitisha dhamira yake ya kudumu ya kuwatumikia wateja wake kwa ubora, kuboresha huduma, na kuhakikisha kila mteja anahisi kuthaminiwa. Kampuni hiyo imejipambanua katika kutoa suluhisho za mawasiliano na kidijitali zinazolenga kurahisisha maisha ya Watanzania.

Kaulimbiu ya “Mteja Kwanza” inaendelea kuwa dira inayoongoza kila huduma, mradi, na uamuzi unaofanywa na Airtel Tanzania.