December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake

Bakari Lulela, Timesmajira Online,Dar

Fatuma Mwandege Mkazi wa Majumbasita Ukonga jijini Dar es salaam, amefanikiwa kutwaa bodaboda katika wiki ya kwanza ya promosheni ya Santa mizawadi.

Akizungumza katika droo hiyo pamoja na kutaja washidi ambapo droo imechezeshwa Desemba 24,2024,Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo, Jackson Mmbando, amesema zawadi ya luninga inchi 55 imekwenda kwa Halima Kimaro wa mkoani Shinyanga.

Andrew Chiomo ambaye ni mwendesha bodaboda mkazi wa Ifakara mkoani Morogoro amefanikiwa kuondoka na kitita cha million 1 na zawadi ya router kutoka Airtel ya kiwango cha 5G imechukuliwa na Josephine Mgagula Mkazi wa Nzega Tabora.Huku zawadi ya simu ya mkononi aina ya ‘smart phone’ imekwenda kwa Omari Ramadhani Mkazi wa Shinyanga.

“Droo hii itafanyika kila Jumanne ya wiki kwa lengo la kuwapa wateja wetu zawadi mbalimbali ikiwemo bodaboda, luninga, Smart phone kwa wale ambao watatumia huduma zetu kwa njia tofauti tofauti,”.

Amesema promosheni ya Airtel Santa mizawadi inalenga kuwashukuru wateja na mawakala waaminifu wanaoendelea kutumia mtandao huo msimu huu wa sikukuu.

Akielezea jinsi ya kushiriki na kujishindia mizawadi ya Airtel Santa mizawadi Mmbando amesema kuwa wakala wa Airtel anatakiwa kufanya miamala ya kuweka na kutoa na kwa wateja wanachotakiwa kufanya ni kununua bando , kulipia bili, kutuma na kutoa pesa na kununua muda wa maongezi au vifurushi.