December 1, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Airtel yashiriki maonesho ya wadau wa Mawasiliano

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Mheshimiwa Naibu waziri Mawasiliano Mhandisi Kondo Mathew ametembelea banda la Airtel katika viwanja vya bunge ikiwa ni siku moja kabla ya kusomwa kwa bajeti ya sekta ya Mawasiliano na kukutana na meneja uhusiano Airtel Jackson Mmbando.
Waziri wa michezo Mheshimiwa Pindi Chana (MB) ni mmoja wa wageni waliotembelea banda la Airtel katika viwanja vya bunge na kuipongeza Airtel kwa mpango wake juu ya uwepo wa simu janja za mkopo kwenye maduka yote nchini. Airtel inaompango wa kutanua wigo wa matumizi wa simu janja (smartphone) kwa kuweka mpango bora wakukosha simu na kulipia kidogo kidogo kwa gharama ya hadi elfu 7 kwa wiki.
Mwandishi Mkongwe wa habari za picha bw, Deus Mhagale akipata maelezo kuhusu Vifaa vya home INTERNET vya Airtel Vinavyoweza kuunganisha hadi watu/vifaa 32 kwa Wakati mmoja kwenye viwanja vya bunge leo ambapo Airtel Wapo kwenye maonesho ya wadau wa Mawasiliano.
Mbunge wa Mbulu Vijijini Mheshimiwa Fratery Massay akipata maelekezo toka kwa watoa Huduma wa Airtel Wakati wa maonesho ya wadau wa Mawasiliano katika viwanja vya bunge leo ambapo Airtel wamehudhuria wakingoja kusoma kwa bajeti ya Mawasiliano hapo kesho.