Na Mwandishi Wetu,TimesMajira Online, Katavi
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kupitia kampeini maalum ya kusaidia jamii kwa ambayo inalenga kuwanufaisha watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu, leo imetoa msaada wa vyakula kwa kituo cha watoto yatima cha Mtakatifu Yohana Paul cha mkoani Katavi.
Kampeni hiyo ya wafanye watabasamu, ilizinduliwa mwishoni mwa mwaka jana na inalenga kunufaisha vituo 12 vya watoto yatima hapa nchini.
Akiongea mara baada ya kutoa msaada huo kwa kituo hicho cha Mtakatifu Yohana Paul, Mkuu wa Mauzo Airtel Mkoa wa Katavi Bartholomew Masatu amesema muda mrefu imekuwa na utamanduni wa kusaidia jamii na kwa kipindi cha msimu wa sikukuu, kampuni iliona ni vyema ikatumia kwa kusherehekea na watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu.
“Leo ni siku yenye furaha sana kwetu zote kwani mayatima ni sehemu ya Jamii yetu na ni muhimu kuwapa upendo pamoja na kuwafariji. Hiki ambacho tumekuja kutoa leo hapa ni kidogo lakini nina uhakika kitagusa mioyo yenu lakini zaidi ni kujua tuko pamoja nanyi na tunawajali sana, amesema Masatu.
Tunayo furaha kuweza kuwafikia watoto hawa ambao wako kwenye kituo hiki na dhamira yetu ni kuendelea kugusa maisha ya watoto wanaoishi kwenye mazingira mangumu na kuwafanya wajisikia kuwa sehemu ya familia ya Airtel, aliongeza Masatu.
Kwa upande wake, Mama Mkuu wa kituo cha Mtakatifu Yohana Paul Sista Rose Sungura amesema ni furaha kwa kampuni kubwa ya Airtel kuguzwa na maisha ya watoto wanaoishi kwenye kituo hiki na hatimaye kuja kutoa msaada na kutuunga mkono.
“Najua kuna vituo vingi vya mayatima hapa nchini kama sisi hapa. Kuamua kuja kuwa na sisi ni Baraka kubwa kwetu. Nachukua fursa hii kuwapongeza wote kwa kile mlichotoa ambacho mnaweza kudhani ni kidogo lakini kinaleta matumaini makubwa kwetu na hasa kwa hawa watoto.
“Naomba kuwakaribisha tena hapa na sio lazima kuja kutoa msaada, lakini mnapokuja kujumuika na hawa watoto wanapata faraja kubwa na kujisikia kama sehemu ya Jamii kwani wengi wao hapa hawajawahi kuona Wazazi wao,” amesema Sungura.
More Stories
Elon Musk : Bill Gates atafilisika endapo…
CRDB yazindua matawi Majimoto, Ilula kuwahudumia wananchi
Lina PG Tour yafufua gofu Moshi