Na Esther Macha, TimesMajira, Mbeya
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya, imemuhukumu kwenda jela miaka 30 mkazi Kijiji cha Izumbi Kata ya Sangambi wilayani Chunya mkoani hapa, Solo Rashid (43) baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka na kumwingilia kinyume na maumbile bibi mwenye umri wa miaka 70.
Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Zawadi Laizer baada ya kuridhishwa na upande wa ushahidi uliotolewa mahakanai hapo na pande zote mbili bila kutia shaka yoyote.
Hakimu huyo amesema mahakamani hapo, kuwa ushahidi umedhihirishwa wazi kuwa mtuhumiwa alimbaka bibi huyo na kumwingilia kinyume cha maumbile, kosa ambalo ni kinyume cha makosa ya jinai hapa nchini.
Kwa upande wa Jamhuri ukiongozwa na Mwanasheria wa Serikali, Davice Msanga aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mtuhumiwa ili iwe fundisho kutokana na watu wengi katika jamii, kuendekeza vitendo visivyofaa na kuhusisha imani za kishirikina.
Ilielezwa mahakamani hapo kuwa, mtuhumiwa alitenda kosa hilo Juni 16 mwaka jana na mshtakiwa alifikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka matatu likiwepo la kuvUnja, kubaka na kulawiti na hivyo kumsababishia maumivu makali mlalamikaji.
Hata hivyo upande wa Jamhuri, uliridhishwa na ushahidi uliotolewa mahakamni hapo dhidi ya mtuhumiwa na hivyo kumpatia adhadu ya kutumikia kifungo chamiaka 30 jela ili iwe fundisho kwa watu wengine.
Kwa upande wake, mtuhumiwa aliiomba mahakama kumpunguzia adhabu ambapo ombi lake lilitupiliwa mbali kutokana na kosa hilo kukinzana na kifungu cha sheria namna 130(1)(2) cha mwenendo wa makosa ya jinai kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
More Stories
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa
NLD kipo tayari kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa