November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Afritrack yatambulisha mfumo wezeshi matumizi ya umeme

Na David John timesmajira,online

MENEJA Mkuu wa Kampuni ya Afritrack, Ashraf Mukri amesema Kampuni yao imekuja na mfumo wezeshi wa kufuatilia matumizi ya umeme katika majengo ya upangishaji ,Ofisi na makazi kwa lengo la kupunguza gharama za matumizi ya thamani zao za majumbani.

Amesema kuwa kama wateja watatumia vifaa vinavyotokana na kampuni hiyo wataondoa wizi wa vifaa vinavyotumika viwandani na hata majumbani kutokana na teknolojia hiyo.

Hayo yamesemwa Novemba 4 mwaka huu jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere JNICC kwenye maonyesho ya ujenzi yanayoendelea ambapo Maneja huyo amesema kuwa mfumo huo unarahisisha kubaini matumizi sahihi ya umeme na kuleta nafuu kwa mtumiaji ikiwa pamoja na kuondoa migogoro kati ya mpangaji na mmiliki wa jengo.

‘’Kwa wale watu ambao wanapangisha nyumba au ofisi wanaweza kutumia mita zetu hasa za umeme ambao wateja watapa mfumo wezeshi kwenye simu na kwa kutumia simu hiyo watanunua umeme na kulipia umeme na kujua umeme kiasi gani umebaki katika mita.’’

Afisa Mauzo wa Afritrack Gabriella Faith akimsikiliza mteja aliyetembelea banda lao lililopo  kwenye ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere JNICC

Ashraf amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa kampuni hiyo wamefikisha miaka 15 na katika miaka hiyo wameshapata tuzo mbalimbali kutoka kwenye kampuni tofauti tofauti na wateja wao ni wale ambao wanapangisha majengo.ofisi.

Meneja huyo amefafanua kuwa yaliyokuwa majengo ya makazi na majengo ya biashara hivyo badala ya kuweka mita kwa kila mpangaji wanaweza kuweka mita moja kubwa ambayo inasimamia umeme wa jengo na kila mpangaji atapewa mita yao ya kufuatilia matumizi ya umeme huo.

Amesema lazima ikumbukwe kuwa kila jengo linaumeme wa tanesco la umeme wa jenereta hivyo kinachofanyika ni jenereta watu wanalipia pesa kiasi Fulani na kwa watu wanaofanya shughuli za ujenzi au biashara inayotumia umeme wanayo pia mfumo wa unaoweza kufanya kazi vizuri.

‘’Hivyo kwa kutumia mifumo yetu ni suluhisho la kuondoa migogoro inayojitokeza katika majengo makazi, ofisi pamoja na sehemu za majengo ya biashara ‘’