December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mgombea wa urais Jamhuri ya Muungano Tanzania Queen Cuthbert Sendiga

ADC: Tujihadhari na wanasiasa wanaoleta sera za uvunjifu wa amani

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online, Pembe

Mgombea wa urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Queen Cuthbert Sendiga

MGOMBEA wa urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniakwa tiketi ya Chama Allance for Democratic Change (ADC), Queen Cuthbert Sendiga amesema endapo atachaguliwa kuwa rais atahakikisha kuwa wananchi wa Pemba wananufaika na zao la karafuum kwa kulipandisha thamani.

Baadhi ya wanachi wakimsikiliza mgombea urais wa Chama Allance for Democratic Change (ADC), Queen Cuthbert Sendiga katika mkutano wa hadhara uliofanyika Micheweni Pemba.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara jana amesema kuwa kwa kufanya hivyo itachangia kuwaingizia fedha za kigeni na kuwafanya wananchi hao kuwa na maisha bora na kufurahia kuwepo kwa zao hilo.

Mgombea huyo amewahidi wanachi kuwa kama watamchangua atahakikisha wanapatiwa viwanda vya kusindika samaki ili kuweza kupata ajira za kutosha katika visiwa hivyo, na kuwaondoa wananchi wa Pemba katika lindi la umasikini.

“Hasa wananchi wa Micheweni ambao kwa takwimu za kitaifa inaonesha wilaya hii ni masikini ya kutupwa hivyo ADC itafanya jitihada Za makusudi kuhakikisha wananchi hao wanaondokana na umasikini,” amesema.

Katika kuhakikisha wananchi wanapata afya ya kutosha hasa kupunguza vifo vya mama na mtoto ADC itawekeza katika sekta ya afya kwa upande wa Zanzibar ili kuhakikisha wananchi hao wanaondoka na kuzorota kwa afya zao.

Zaidi amewaasa wana Micheweni na Watanzania wote kujihadhari na wanasiasa wanaoleta sera za uvunjifu wa amani,Queen amesema wanasiasa hao waogopwe kama Corona na amesisitiza kulinda amani ni jukumu la kila Mtanzania.

Mgombea huyo anaendelea na kampeni zake kesho katika Mkoa wa Tanga katika Wilaya ya Korogwe, Handeni pamoja na Kilindi.