January 27, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

ACT-Wazalendo Zanzibar wafungua mkutano mkuu wa uchaguzi wa chama hicho

Na Mwandishi Wetu,Timesmajiraonline,Dodoma

MAKAMU Mwenyekiti wa ACT – Wazalendo Zanzibar, ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,Othman Masoud Othman, leo Jumamosi Januari 13, 2024 amewaongoza Viongozi mbali mbali, katika Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi, wa Chama chake, Mkoa wa kichama wa Kaskazini ‘A’ Unguja.

Hafla hiyo  ambayo imefanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Mafunzo ya Amali Mkokotoni, Mkoa wa Kaskazini Unguja, ni Mfululizo wa Mikutano anayoendelea kuiongoza Mheshimiwa Othman, ili kufanikisha Zoezi la Uchaguzi wa Ndani ya ACT-Wazalendo, Nchini kote.

Kwa upande wa Kaskazini Unguja, Mkutano huo wa Uchaguzi una dhamira ya kuwapata Viongozi Wapya watakaokitumikia Chama hicho kwa Kipindi cha Miaka Mitano (5) ijayo, katika Ngazi ya Mkoa.

Katika Mkutano huo  wamehudhuria pia Mjumbe wa Kamati kuu ya Chama Ndugu Hassan Jani Masoud na Katibu wa Uchaguzi Ndugu Muhene Said Rashid.