March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

ACT Wazalendo yajipanga kushika dola

Na Heri Shaaban,Timesmajira Online-Dar es Salaam)

CHAMA cha ACT Wazalendo kimesema wapo vitani kurejesha heshima ya kulinda kura na demokrasia ili washike dola katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu.

Akizungumza katika mkutano Mkuu wa chama ACT Wazalendo, kiongozi wa chama hicho Dorothy Semu ,amesema chama hicho kimejipanga vizuri kuhakikisha wanadhibiti hujuma ili kishike dola pamoja na kufanikisha malengo yao ya kisiasa

Amesema,ACT Wazalendo wanafufua ari ya mapambano na kusonga mbele hadi kupata ushindi kwa mshikamano wao ili kufikia malengo yao.

Semu,amesema wanashiriki uchaguzi mkuu kwa dhamira ya wananchi ili waweze kuchagua nani awe kiongozi wao wa kuwatumikia katika kuleta maendeleo.

Pia amedai kiwa Serikali imeshindwa kusimamia uchumi,huduma za jamii na masuala ya utawala bora kupelekea watanzania kuishi katika umasikini na ukosefu wa ajira na uhakika wa vipato wakiwa hawana huduma bora za kijamii .