Na MwandishiWetu, Timesmajiraonline,Geita
JIMBO la Geita Mjini ni miongoni mwa majimbo ya uchaguzi nchini yaliyokuwa na ushindini mkubwa kwenye kura za maoni kwa ajira ya kuwapata mgombea ubunge wa kupeperusha bendera ya CCM katika Uchaguzi wa Mkuu wa mwaka 2020.
Miongoni mwa waliokoleza ushindani huo ni vijana waliotia nia kwenye mchuano huo, huku baadhi yao wakionekana kuwa na ushawishi na uwezo mkubwa wa kuliongoza jimbo hilo, japo ilikuwa ni mara yao ya kwanza kwenye kinyang’anyiro hicho.
Pamoja na ushindani mkubwa kwenye kura za maoni ndani ya CCM, aliyeibuka mshindi alikuwa, Constantine Kanyasu, ambaye ndiye mbunge wa sasa wa Geita Mjini.
Wakati huu wa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, mwaka huu tayari joto la kisiasa limeanza kupanda ndani ya jimbo hilo miongoni mwa wana CCM.
Kadri siku zinavyosogea, ndivyo vugu vugu linavyozidi kupamba moto, huku baadhi ya wana-CCM wakianza kuwapigia chapuo wale wanaoonekana kuwa na uwezo mkubwa wa kuliletea maendeleo jimbo hilo kwa kuendelea mbele zaidi alipofikia mbunge wa sasa.
Miongoni mwa wana CCM vijana wanaoshawishiwa wajitose kuwania ubunge ni kijana, Abdullah Rashid Barre. Barre ni miongoni mwa wagombea 39 walioshiriki kinyang’anyiro cha mwaka 2020 ndani ya CCM, katika kura za maoni, lakini kura hazikutosha.
Hata hivyo, bado wana-CCM wana imani kubwa na Barre wakitamani kumuona anajitosa kuomba kusimamishwa na chama chake (CCM) kuwania nafasi hiyo kwa kile wanachoeleza kuwa ni kijana mzalendo na mwenye maono makubwa ya maendeleo kwa Jimbo la Geita Mjini na nchi kwa ujumla.
Mmoja wa wana-CCM akizungumza kwa sharti la jina lake kutochapishwa gazetini, anasema anapenda kumuona Barre anawania ubunge ili kulihudumia Jimbo la Geita Mjini na wananchi kwa ujumla.
“Muda utakapofika kwa mujibu wa taratibu za kichama, tunatamani kuona kijana huyo anatumia haki yake ya kikatiba kuchukua fomu ya kuomba ridhaa kupitia CCM ili awatumikie wananchi wa jimbo la Geita Mjini.”Anasema na kuongeza;
“ Tuna dhamira ya dhati ya kuona kijana huyu anatumia ujuzi na elimu aliyonayo kwa manufaa ya wananchi wa Geita Mjini na kuwasaidia vijana wanaohitaji fursa, msaada wa kitaaluma na uelewa wa masuala ya kiuchumi, kijasiriamali na kijamii.”
Alisema wanatamani kuona kizazi kipya kinapewa nafasi, kinawezeshwa na kuaminiwa.”
Mwachama mwingine wa CCM (jina tunalo) anasema kwa anavyomfahamu Barre akipitishwa na CCM na kushinda jimbo hilo, watakuwa wamelamba dume
“Kwa tuliyemuona mwaka 2020 wakati wa kura za maoni kijana huyo (Barre) si tu anajitambulisha kama kiongozi kijana, bali ana ndoto ya maendeleo, anaonekana wazi amejipanga kutumia uzoefu na elimu aliyonayo kuibadilisha Geita Mjini kuwa kitovu cha mafanikio ya vijana, uchumi wa kati na ustawi wa kijamii,” anasema.
Mwana CCM huyo anasema Barre alipochukua fomu ya kugombea ubunge wa Jimbo la Geita Mjini kupitia CCM mwaka 2020, hatua ilidhihirisha dhamira yake ya dhati ya kulitumikia taifa na wananchi wa Geita kwa moyo wa kizalendo na maono ya maendeleo jumuishi.
“Kupitia hatua hiyo, alionesha kuwa si tu mwanasiasa kijana mwenye malengo, bali pia mtu mwenye uthubutu wa kuchukua jukumu la kuleta mabadiliko chanya katika jamii yake,” anasisitiza mwana CCM huyo.
Kwa mujibu wa wana CCM katika Jimbo la Geta Mjini pamoja na kura za Barre kutokusha mwaka huo 2020, hajakata tamaa, kwani mchango wake jimbo la Geita na Taifa kwa ujumla umekuwa mkubwa kwa uungaji Mkono kwa Jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan
“Kijana huyu ameendelea kuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia, katika kuwaletea wananchi maendeleo endelevu.
Akiwa kijana mzalendo na kiongozi mwenye dira, amekuwa akihamasisha jamii, hususan vijana kutambua na kushiriki kikamilifu katika juhudi za ujenzi wa taifa zinazoongozwa na Serikali ya Awamu ya Sita.” Anasema kada wa CCM, Robert Paul.
Paul anasema kupitia mikutano ya vijana, makundi ya kijamii, na majukwaa ya elimu, Barre amekuwa akieneza ujumbe wa mshikamano, uzalendo na ushiriki wa pamoja katika utekelezaji wa Ilani ya CCM.
Anatoa mfano akisema, Barre akiwa Mwenyekiti wa Kikundi cha “Sauti ya Samia” mkoani Geita, amekuwa kiungo muhimu katika kutoa elimu juu ya mafanikio ya Serikali ya Rais Samia na kushirikisha wananchi katika mchakato wa maendeleo.
“Kwa maono yake ya uongozi unaojali watu na uaminifu kwa chama chake, Barre anaendelea kuwa sauti ya matumaini kwa kizazi kipya, akisisitiza kuwa ni jukumu la kila Mtanzania kuunga mkono dira ya Rais Samia kwa vitendo,” anasema Paul wakati akieleza jinsi anavyomfahamu Barre.
Kada huyo wa CCM anasema tangu alivyofahamiana na Barre wakiwa chuoni ameendelea kushiriki kikamilifu kwenye masuala ya kisiasa na kijamii.

“Ameendelea kuwa sauti muhimu katika kuhamasisha wananchi wa Geita Mjini kushiriki ipasavyo katika masuala ya uraia. Amekuwa mstari wa mbele kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye Daftari la Wapiga Kura, hususan vijana wanaofikia umri wa kupiga kura kwa mara ya kwanza,” anasema.
Aidha, Paul anasema Barre amekuwa akiimiza vijana kushiriki kwenye uchaguzi kwa amani, kuhakikisha kila mmoja anatumia haki yake ya kikatiba kuchagua viongozi wanaofaa.
Naye Anna Daud anasema kijana huyo amekuwa kama sehemu ya mfumo wa utawala bora, kwa kuwahamasisha wananchi kuwa wachangiaji wa maendeleo kwa kushiriki vikao vya kisheria na mijadala ya kijamii.
“Hiyo imemjengea umaarufu mkubwa hasa kwa kuzingatia kuwa amekuwa akihamasisha wanawake kushiriki kwenye uongozi, akiamini katika usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa makundi yote katika jamii,” anasema.
Anasema Barre ndiye aliyemfanya yeye na vijana wenzake kujua haki za makundi maalum kama vijana, wanawake, na watu wenye ulemavu kupitia elimu ambayo amekuwa akiwapa.
“Hiyo imetufanya kujua haki haki zetu, fursa za maendeleo, na wajibu wetu kwa taifa,” anasema.
Anafafanua kuwa kupitia majukwaa mbalimbali na vikundi vya kijamii, Barre ameendelea kuwa chachu ya mwamko mpya wa kisiasa, akilenga kuona jamii ya Geita Mjini inayoshiriki kikamilifu katika maamuzi ya mustakabali wao.

More Stories
Ndoa za utotoni kikwazo kufikiwa usawa wa kijinsia
Tanzania bado inanafasi ya kupunguza matumizi ya Trans Fat Acid katika Vyakula
Usajili wa Laini: Utambulisho Wako na Usalama Wako