March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Regina: Tupigieni kura,mtudai maendeleo baada ya uchaguzi

Judith Ferdinand, Timesmajira Online-Mwanza

Mgombea Udiwani wa Kata ya Pasiansi jimboni Ilemela mkoani Mwanza kupitia Chama Cha Mapindizi(CCM),Regina Lubala,amewaomba wananchi wa Kata hiyo kuwapigia kura wagombea wanaotokana na chama hicho akiwemo yeye.

Na baada ya uchaguzi unaotarajia kufanyika Oktoba 29,2025,wananchi wakawadai maendeleo kwa viongozi haon akiwemo Diwani ambaye ni yeye endapo atashinda.

Regina amezungumza hayo Oktoba 5,2025, katika mkutano wa kampeni uliofanyika mtaa wa Pasiansi Juu, jimboni Ilemela,ambapo amesema wananchi wa Kata hiyo wana changamoto nyingi wanazo pitia ambazo zinahitaji ufumbuzi.

Miongoni mwa changamoto hizo kwa upande wa Pasiansi Juu ni pamoja na ubovu wa miundombinu ya barabara ambayo imekuwa kero kwa wananchi pindi wakitaka kwenda kustilihi wapendwa wao kwenye makaburi yaliopo mtaani hapo.

“Katika mtaa huo kuna barabara ambayo inapita mpaka kwenye maeneo ya makaburi tunakohifadhia ndugu zetu, barabara imekatika na kuleta changamoto hivyo inafika wakati magari hayawezi kufika kule chini,hivyo nitakapo kuwa Diwani nitashughulikia suala hilo,”amesema Regina.

Amesema,atashirikiana na wananchi katika kuhakikisha maendeleo ya Kata hiyo yanapatikana.

“Pasiansi mpya itajengwa na Mimi na wewe,nikipata ridhaa ya kuwa Diwani nitashirikiana na nyingi wananchi kuleta maendeleo na kupata Pasiansi mpya na ilio njema,”amesema Regina.

Sanjari na hayo amesema,endapo atapata ridhaa ya kuwa Diwani ataenda kusema suala la upimaji shirikishi uliofanyika mtaa wa Pasiansi Juu lakini wananchi hawajapata hati mpaka sasa.

“Mkinipa tu ridhaa ya kuwa Diwani ni tahakikisha wananchi wa mtaa wa Pasiansi Juu ambao mmepimiwa viwanja mnapata hati zenu ili muwe na amani pamoja na kuhakikisha nishati ya umeme inawafikia wananchi wa mtaa wa Bwiru Elimu,”.

Kwa upande wake mmoja wa wananchi wa mtaa wa Pasiansi Juu,Chacha Mares,amesema,sera za Diwani huyo ni nzuri na endapo atazitekelez kama anavyo ahidi anaiona Pasiansi mpya.