Na Heri Shaaban (Dar es Salaam)
Wazazi wamehimizwa kushirikiana na walimu bega kwa bega ili kuweza kuvikuza vipaji vya watoto wao.
Hayo yalisemwa Dar es Salaam Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kisutu Elizabeth Massawe ,wakati wa siku ya maonesho ( Exhibition day) kwa Wanafunzi wa elimu ya Awali , darasa la kwanza,la pili na la tatu iliyofanyika katika ukumbi wa Shule ya Msingi Kisutu Jijini Dar es Salaam iliyokwenda sambamba na mahafali ya darasa la awali.
Mwalimu Elizabeth Masawe alisema maonesho hayo ni fursa ya kuthibitisha kuwa elimu ya awali si msingi wa tu wa maarifa bali ni chachu ya ya kuibua uwezo wa mtoto kwa njia ya maarifa kwani watoto ni mbegu wanazopanda kwa matumaini ya mavuno bora ya kesho.

Mwalimu Massawe pia amewapongeza walimu na wazazi kwa kazi kubwa na nzuri ya kuwalea watoto hao kielimu na kiakili kupitia kazi zao za Sanaa ikiwemo michezo ya kuigiza,nyimbo, maonesho ya sayansi na lugha.


More Stories
TAMWA yakumbusha jamii kupinga ukatili wa kijinsia kuelekea siku ta wanawake Duniani
Wanawake washauriwa kuchangamkia fursa za uchumi
Aida:Wanawake wakipata haki zote itapunguza migogoro