Na Mwandishi Wetu Timesmajira Online
KATIKA jitihada za kuongeza upatikanaji wa simu za mkononi na kukuza matumizi ya huduma za kidijitali nchini Tanzania, Kampuni inayoongoza kwa huduma za kidijitali, Yas ikishirikiana na ZTE, imezindua rasmi simu mpya aina ZTE Blade A36 na ZTE Blade A76.
Simu hizo mpya zinachukua nafasi ya matoleo ya awali, ZTE A35 na A75, zilizozinduliwa mwaka 2024 na kuwa chachu ya upatikanaji wa teknolojia ya simu nchini.
Matoleo mapya yanakuja na kamera zilizoboreshwa, utendaji ulioimarishwa, na chaguzi rahisi za ununuzi, zikilenga kufanya teknolojia ya kisasa ya simu iweze kufikiwa na mamilioni ya Watanzania.
Kupitia ushirikiano huu, simu hizo zitapatikana kwenye maduka yote ya Yas kote nchini kwa njia ya malipo ya fedha taslimu au kupitia mpango wa malipo ya mkopo.

Wateja watakaotumia mpango wa mkopo wanaweza kulipa ndani ya miezi 6 au 12, malipo ya chini yakiwa Tsh. 700 kwa siku, ikiambatana na bando la masaa 24 kila siku. Hivyo Wateja wa malipo ya fedha taslimu watapata bando la kwa mwaka mzima.

Akizungumzia hilo, Meneja wa Vifaa na Huduma za Interneti Imelda Edward, alisema kupitia ushirikiano wao na ZTE kuleta Blade A36 na A76 sokoni, wanawezesha Watanzania kushiriki kikamilifu katika uchumi wa kidijitali, kupata huduma muhimu, na kuungana na dunia.
“Simu hizi ni hatua nyingine ya dhamira yetu ya kubadilisha maisha ya Watanzania kupitia teknolojia.” Amesema.

Naye Meneja Mkaazi wa ZTE, Duan Cunxin amesema Tanzania ni soko linalokua kwa kasi lenye fursa kubwa za mabadiliko ya kidijitali.
Amesema, Kupitia ushirikiano huo na Yas, wamezindua simu zinazounganisha bei na utendaji, kuhakikisha Watanzania wengi wanaweza kufurahia maudhui mitandaoni na huduma za kidijitali.
“Uzinduzi huu unafuatia ongezeko la mahitaji ya intaneti ya simu nchini, ambayo tayari yameongezeka kwa asilimia 36.75.

“Simu hizi, zenye bei ya chini na kati, zinatarajiwa kushindana sokoni kutokana na ofa za mikopo ya kipekee ambayo haipatikani kwa watoa huduma wengine,” amesema.
Kwa mpango huo, Yas na ZTE wanajiweka mstari wa mbele katika mapinduzi ya simu za mkononi nchini, wakilenga kuunganisha Watanzania wengi zaidi, kuhamasisha matumizi ya data, na kuendeleza mtindo wa maisha ya kidijitali kwa wote.

More Stories
Wanawake jumuia ya kikristo Tanzania CCT wafundana kuelekea siku ya Wanawake Duniani
Dkt.Tulia,Mwalunenge waungana kutatua changamoto ya barabara
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi