Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online-Dar
SHULE ya sekondari Benjamin Wiliam Mkapa iliyopo wilayani Ilala,imejivunia mafanikio kitaaluma kwa miaka minne kuanzia mwaka 2021 hadi 2024.
Akizungumza katika mahafali ya 25 ya kidato cha nne ya sule ya Benjamini William Mkapa,Mkuu wa shule hiyo Joseph Deo, amesema katika kipindi cha miaka minne imekuwa na matokeo mazuri kwa mitihani ya kidato cha nne.

Ambapo kwa mwaka 2021 ufaulu ulikuwa asilimia 97, mwaka 2022 ufaulu asilimia 97, mwaka 2023 ufaulu asilimia 98 na mwaka 2024 ufaulu asilimia 98.
“Tunaamini kwa jitihada za walimu na wanafunzi mwaka 2025 tutapunguza daraja 0,na tumejipanga angalau wanafunzi 100 wapate daraja la kwanza,”amesema Mwl. Deo.
Sanjari na hayo Mwl. Deo,amesema shule hiyo ilianzishwa mwaka 1998 kwa jina la City High school na mwaka 1999 ulinzinduliwa rasmi na Hayati Benjamini William Mkapa na kuitwa Benjamini Mkapa.

Mpaka sasa ina wanafunzi 1476, kati yao wa kike ni 632 na wakiume 844,wakiwemo wenye mahitaji maalumu na kwa mwaka huu wanafunzi 156 wanatarajiwa kuhitimu kidato cha nne.

More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi