March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Halo pesa yaja na Mr. Bonasi Tamba na bonasi kwa kufanya miamala

Na Bakari Lulela,Timesmajira

KAMPUNI ya mawasiliano ya halotel kupitia huduma yake ya Halo pesa  imezindua rasmi kampeni iitwyo “Tamba na Bonasi” sambamba na utambulisho wa msaidizi wa kidigitali anayejulikana kama Mr. Bonasi ambaye atakuwa kwenye kampeni hiyo.

Kupitia kampeni hii wateja wa halo pesa watapata nafasi ya kujishindia bonasi kabambe ya kuingia kwenye droo za kila siku, kila wiki na kila mwezi kwa kufanya miamala mbalimbali .kupitia halo pesa ikiwa ni pamoja na kutuma pesa, kutoa pesa, malipo ya bili na bidhaa ya kununua umeme ( LUKU) ambapo wateja watajipatia nafasi ya kushinda hadi shilingi milioni mbili.

Hata hivyo halo pesa inawapa urahisi wateja wanapofanya miamala ya Halo pesa kwenda halo pesa ni Bure kabisa bila ya makato kupitia Halo pesa App, lakini pia kununua Luku kupitia Halo pesa App ni Bure. Ni mwendo wa kuserereka.

Akizindua kampeni hiyo, Mkuu wa idara ya biashara Halo pesa Happy Mzena amesema kwamba uzinduzi huo ni sehemu ya mikakati wao wa kuendelea kutoa thamani zaidi kwa wateja wao. 

Mr . Bonasi siyo tu nembo ya kampeni hii bali ni jukwaa la kidigitali la zawadi linaloleta msisimko katika kila miamala. Lengo letu ni kufanya kila huduma ya Halo pesa kuwa ni fursa kwa wateja wao
“Tunatoa wito kwa wateja wetu waendelee kufanya miamala kupitia Halo pesa, ikibidi waweze kutambua zaidi na bonasi na huenda ukawa mshindi wa zawadi kubwa kutoka kwa Mr. Bonasi,”amesema Mzena

Kwa upande wake, Afisa masoko wa Halo pesa Aidat Lwiza alieleza kwa kina ubunifu na thamani ya kampeni hiyo.
“Tamba na bonasi ni uzoefu wa kipekee wa kidigitali uliobuniwa kwa ajili ya wateja wetu wa halo pesa. Mr bonasi amekuja kuleta msisimko mpya, akiwaletea wateja zawadi kwa njia ya kipekee, kirahisi na ya kupitia teknolojia ya kisasa ambapo wateja wetu wanaweza kujishindia kila wanapofanya miamala ya kila siku,”

“Tunaamini kuwa huduma za kifedha hazipaswi kuwa  rahisi na salama Bali pia kuwa na mvuto, thamani ya nyongeza na zawadi. Halo pesa imeendelea kuwa kinara sokoni kwa kutoa makato nafuu zaidi ukilinganisha na huduma nyingine, huku ikijivunia kuwa na huduma bora kwa wateja nchi mzima. Tuna Mtandao mpana wa mawakala na maduka ya halotel kote nchini, kuhakikisha kila mtanzania anapata huduma bila ya usumbufu,”

“Zaidi ya yote kupitia kampeni hii maelfu ya wateja wanapata nafasi ya kujishindia na kushine na Mr. Bonasi kila siku, kila wiki na kila mwezi tunawakaribisha watanzania wote kujiunga na Halo pesa kwa sababu sasa kila muamala sio tu njia ya kutumia au kupokea fedha bali ni hatua moja kuelekea ushindi halisi.,” amesema Aidat

Aidat ameendelea kuhimiza umuhimu wa Usalama wa taarifa binafsi kwa wateja wakati wa kampeni hii.Taarifa zote za ushindi zitatumwa kupitia ujumbe rasmi wenye jina la Halo pesa tu na simu zozote kutoka kwetu zitatoka kupitia huduma kwa wateja 100.