Na Penina Malundo,Timesmajira
MKUU wa Chuo cha Ulinzi wa Amani Tanzania (TPTC),Brigedia Jenerali George Itang’are amesema jumla ya Polisi Jeshi 125 wanatarajia kwenda kutekeleza majukumu yao ya Ulinzi wa Amani chini ya Umoja wa Mataifa nchini Lebanon.
Aliyasema hayo leo Septemba 17,2025 jijini Dar es Salaam,wakati wa kuwaaga walinzi hao wa amani na kusema kuwa Polisi Jeshi hao wanatarajia kwenda nchini humo kwa kipindi cha Mwaka Mmoja kwa mujibu wa utaratibu wa Jumuiya ya Umoja wa Mataifa.
”Leo tulikuwa na tukio muhimu la kuwaaga walinzi wa amani wanaotarajia kwenda kutekeleza majukumu yao ya
Kikundi hiki ambacho kinaundwa na kombaniambili za Polisi Jeshi.
”Kikundi hiki kilikuwa kwenye mafunzo tangu Mwezi wa nne,sasa wamekamilisha mafunzo na sasa wapo tayari kwenda kwenye majukumu ya ulinzi wa amani nchini Lebanon.
Amesema kikundi hicho cha Jeshi cha Polisi Jeshi ni cha kwanza kwenda chini ya Umoja wa Mataifa tangu walipopelekwa kule mwaka 2007.”Umoja wa mataifa umekuwa na imani kubwa sana na utekeezaji wa majukumu yake na ndio sababu ya kuongeza ushiriki wa Tanzania katika maeneo mengi.

”Tumeweka historia kubwa kuendelea kufanya kazi kwa uaminifu mkubwa,na kwa bahati nzuri hakuna tukio lolote la uvunjifu wa nidhamu toka tuanzishe haya,”amesema.
Ametoa ujumbe wake kwa Polisi hao kuwa Mkuu wa majeshi anasisitiza,Wanajeshi waishi kwa viapo vyao hivyo wanatarajia huko wanapoenda watapeperusha bendera ya Tanzania na ya Umoja wa Mataifa ipasavyo kwa weledi na kuhakikisha wanalinda mamlaka nguvu ya umoja wa mataifa kama ilivyotolewa.

Kwa upande wake Mkuu wa Kombani ya Polisi Jeshi kundi la 33/34-2025,Luteni Kanali Abdallah Hussein Rajab amesema kulingana na maelekezo waliyopewa na Makao Makuu ya Jeshi wamejipanga kwenda kutekeleza majukumu ya umoja wa mataifa kulingana na azimio walioanzisha misheni ya Lebanon toka mwaka 1978.

”Sisi tumejipanga kwanza kwenda kutekeleza maagizo au amri tuliyopewa na Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi Tanzania pia kutekeleza maazimio ya umoja wa mataifa kupitia operesheni wanayoenda kufanyia kazi,”amesema.
Kapteni Fatuma Adam Miongoni mwa wanajeshi wanaoenda nchini Lebanon Kulinda Amani amesema wao kama wanawake walichojipanga nacho ni kwenda kutekeleza majukumu yote ambayo yameainishwa na Jeshi pamoja na majukumu yote yaliyoainishwa na Umoja wa Mataifa.

”Tutakachokifanya huko ni kushirikiana na wenzao na kuhakikisha kwamba amani inaendelea kuwepo na kuwasaidia wanawake wanapokuwa katika majukumu yao.
”Changamoto zipo hususan kwa waathirika wa vita lakini tutajitahidi kupambana nazo kuziweka sawa,”Amesisitiza.

More Stories
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI