Na Agnes Alcardo,Timesmajira
Mke wa Mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi, Jane Nchimbi, amemuombea kura za ndiyo Rais Samia, kwa wananchi wa Tanga, akiwaomba kumpigia kura kwenye Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025.
Jane Nchimbi, amewaomba wananchi hao kumpigia kura Rais Samia, kwenye mkutano uliofanyika leo Septemba 15, 2025 katika Uwanja wa Mazoezi Mjini Korogwe, Tanga, alipigudhuria kwenye kampeni za Mgombea Mwenza wa Urais zinazoendelea katika Mkoa wa Tanga.

Jane Nchimbi ambaye ni mwenyeji wa Korogwe wakati akisalimiana na wananchi wa Korogwe, alitumia fursa hiyo kuwaomba wananchi hao pia kuipa ushindi wa kishindo CCM.


More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako