Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online+Longido
MGOMBEA Mwenza wa kiti cha Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi,amesema endapo chama hicho kitashika dola kwa mara nyingine,mbali na mambo mengine kitaanzisha mpango wa ardhi wilayani Longido mkoani Arusha.
Akizungumza kwenye mkutano uliofanyika katika Jimbo la Longido,Septemba 12,2025, Jijini Arusha,Dkt.Nchimbi amesema,watahakikisha wanazingatia uboreshwaji wa maeneo mbalimbali kwa kuanzisha mpango wa ardhi ili kuipa hadhi miji na manufaa kwa wakazi husika, pamoja na kuongeza miradi ya maendeleo.

Amesema, vipaumbele vingine ni pamoja na kuboresha upande wa elimu, ambapo katika Wilaya hiyo zitajengwa shule za msingi 26 na shule za sekondari mbili, zitakazokuwa na madarasa 88.
Nchimbi amesema, endapo wananchi wa Longido watakipigia tena kura chama hicho, Serikali chini Dkt. Samia Suluhu Hassan, itaenda kujenga zahanati tano na vituo vya afya vinne.
Pia amesema,Serikali chini ya chama hicho itaenda kuboresha miradi ya maji ikiwemo ujenzi wa mabwawa, majosho 18 ya kuogeshea mifugo,kuongezwa kwa maofisa mifugo, ili kusaidia kutoa huduma za chanjo kwa mifugo na elimu kwa jamii hiyo ya wafugaji, pamoja na kukuza utalii katika Jiji la Arusha.



More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako