*Ili kuwezesha watoto wa kkki
Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online-Dar
WADAU wa maendeleo nchini wameiomba Serikali kuondoa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwenye taulo za kike ili kuwezesha watoto wa kike, hususani waliopo vijijini, kupata pedi salama kwa gharama nafuu.
Ombi hilo limetolewa jijini Dar es Salaam Septemba 10,2025,na Ofisa Uhusiano wa kampuni ya Beneficial Company Limited, Perpetua Mtwale,wakati wa uzinduzi wa taulo za kike za ARI zinazozalishwa na kampuni hiyo.

Ambapo amesema kutokana na gharama kubwa ya uzalishaji na uuzaji wa pedi inaendelea kuwa changamoto kwa watoto wengi wa kike nchini kupata vifaa hivyo vya kijistili wakati wa hedhi.
“Tunaomba Serikali itufikirie sisi wazalishaji wa ndani kwa kuondoa VAT kwenye taulo za kike. Hedhi ni asili, siyo chaguo. Kodi hii ni msiba na kilio kwa wengi,” amesema
Amesema kuwa licha ya kampuni hiyo kufanikisha usambazaji wa pedi katika shule za Dar es Salaam, Pwani na Zanzibar, bado watoto wengi hawawezi kumudu gharama za pedi kwa sababu ya ushuru huo.
Kwa upande wake, Balozi wa Taulo za Ari na Balozi wa Hedhi Tanzania, Najma Paul, ameeleza kuwa kampuni hiyo imejikita si tu kwenye biashara pia katika utoaji wa elimu ya afya ya uzazi.
“Tunatoa elimu, siyo kuuza tu. Tunashirikiana na shule, jamii na wadau mbalimbali kuhamasisha usafi wa hedhi. Lengo ni kuhakikisha mtoto wa kike anakaa shuleni salama bila changamoto ya hedhi,” amesema Najma.

Aidha,amewataka Wabunge na watunga sera kuangalia upya sheria ya VAT ili kupunguza gharama kwa wanawake na watoto wa kike nchini.
Naye Ofisa Masoko wa kampuni hiyo,Erasto Margwe,ametoa wito kwa wanaume kushiriki kuhamasisha elimu ya hedhi salama, akisisitiza kuwa kampuni hiyo inarudisha kwa jamii kwa kugawa pedi bure kwa wenye uhitaji na kutoa elimu kwa wavulana na wasichana kwa pamoja.
“Tunaamini elimu ya hedhi salama ni ya kijamii na kila mtu anapaswa kushiriki kuondoa unyanyapaa na kuongeza uelewa,” amesema Margwe.


More Stories
Wanawake jumuia ya kikristo Tanzania CCT wafundana kuelekea siku ya Wanawake Duniani
Dkt.Tulia,Mwalunenge waungana kutatua changamoto ya barabara
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi