March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dkt.Tulia kuendelea kukuza vipaji, kuleta mabadiliko ya kiuchumi

Na Esther Macha,TimesmajiraOnline,Mbeya

SPIKA wa Bunge na Rais umoja wa Mabunge Duniani(IPU)Dkt.Tulia Ackson amesema  kuwa ataendelea  kukuza na kuibua vipaji kwa vijana kupitia mashindano ya Tulia Trust Cup  ambayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka na kuleta mabadiliko  ya  kiuchumi kwa vijana .

Dkt.Tulia amesema hayo wakati alipokuwa mgeni rasmi katika mashindano ya Tulia Trust Uyole Cup 2025 ambapo amewakabidhi Mabingwa Itezi United,zawadi Shilingi Mil.10 pamoja na Kombe la Ubingwa huku akiahidi kuendelea kudhamini Mashindano hayo Kwa Miaka Mitatu ijayo.

“Ahadi yangu kwenu ni kuendelea kuwatumikia na kuendeleza vipaji vyenu vijana nataka michezo iwe sehemu ya ajira kwenu naamini katika mashindano haya ambayo yamekuwa yakifanyika yameleta mabadiliko kwa vijana walio wengi,” amesema.

Katika mashindano hayo timu ya Itezi United Kutoka Kata ya Itezi Mkoani Mbeya imetwaa Ubingwa wa Mashindano ya Tulia Trust Uyole Cup 2025 baada Ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Timu ya Chipukizi Fc ya Mkoani humo Kwenye Ligi iliyoshirikisha Idadi ya Timu 35..

Zawadi Nyingine zilizotolewa ni kwa Mshindi wa Pili Chipukizi Fc aliyepata zawadi ya Shilingi Mil.5 Mshindi wa Tatu Airport Fc Waliopewa zawadi ya Shilingi Mil.3 Pia zawadi Mbalimbali zimetolewa Kwa Wachezaji waliofanya Vizuri Kipa Bora, Mchezaji Bora, Mfungaji Bora, Timu yenye nidhamu, Mwamuzi Bora (Refa Bora) na Kikundi Bora Cha Ushangiliaji.

Hata hivyo Dkt.Tulia amesema kuwa  Kwa mwaka huu walikubaliana kuongeza zawadi kwa  washiriki wa mashindano hayo  nia ya kutoa zawadi kubwa hizo vijana wanatumia nguvu zao na watazamaji wanaburudika na  kasema kuwa anatamani kuona vijana waone michezo ni ajira.

“Tumeanza kutoa zawadi hizi kubwa kubwa hawa vijana wanaotumia nguvu zao kucheza uwanjani,hivyo tunatamani kuona vijana kupitia michezo waone ni ajira kwa hiyo wajitume na fedha wanayopata waone kama tuweze  kujituma na kujiendeleza na kuwa Uchumi mkubwa “amesema Dkt.Tulia.

Kwa upande wake Mdhamini wa mashindano hayo, Raphael Ndelwa  amesema kutokana na Dkt.Tulia kuwa Mbunge wa Uyole kuangalia namna ya kupunguza gharama za uchaguzi ili  fedha ambazo zilitakiwa kufanyika Kwenye uchaguzi basi  ziende Kwenye mashindano ya mpira wa miguu, pamoja  na kufanya ujenzi wa vyumba vya madarasa, kudumisha  viwanja vya michezo.