Na Agnes Alcardo Timesmajira Online.
MGOMBEA Mwenza wa Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amesema katika siku 100 za mwanzo, itaanzishwa tume ya maridhiano itakayosaidia wananchi wote kusikilizwa kwa usawa, kuleta amani na kudumisha umoja ili watanzania wawe kitu kimoja.
Balozi Nchimbi ameyasema hayo leo, katika eneo la Lalago, Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, wakati akiongea na wananchi katika mkutano, akiomba ridhaa kwa wakazi wa Lalago kuichagua CCM, ili iweze kushika dola kwa kipindi kingine cha miaka mitano ili iendelee kuwaletea maendeleo watanzania.

Pia, Balozi Nchimbi ameelezea mipango ya maendeleo kwa miaka mitano ijayo katika Wilaya ya Simiyu kuwa ni pamoja na ujenzi wa vituo vya afya sita, Zahanati 10, Shule ya Msingi madarasa 100, Sekondari madarasa 200 na Vyumba vya Maabara 75.

Nyingine ni uboreshwaji wa mabomba ya maji vijiji vya Mogwa na Isulile na Skimu za umwagiliaji maji na hekta za umwagiliaji zitaongezwa hadi 500.


More Stories
Mfanyabiashara,vibarua mbaroni wakituhumiwa kuchimba mahandakiÂ
Silinde azindua baraza la sita la Wafanyakazi Tume ya Taifa ya Umwagiliaji
NMB ilivyosaidia Serikali kukusanya zaidi ya Sh trilioni 9.8