Esther Macha, Timesmajira Online-Mbeya
MGOMBEA Udiwani kupitia Chama cha Mapinduzi(CCM)Kata ya Rujewa,Jeremia .Makao, Agosti 27,2025,amerejesha fomu za utezi wa kuwania nafasi hiyo katika ofisi za Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Kata hiyo huku akiahidi kuendeleza pale alipoishia 2020-2025.
Makao alikuwa Diwani wa Kata ya Rujewa kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita huku akipata fursa kwa mara nyingine ya kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29,2025.
“Wananchi wa Kata ya Rujewa tunakwenda kufanyia kazi mambo mbalimbali ikiwemo miundombinu ya barabara, madaraja na elimu,”amesema Makao.
Msimazi Msadizi wa uchaguzi Kata Rujewa,Harrno,Gauday amesema jumla ya vyama vilivyo fomu kwa kiti cha udiwani ni saba ikiwemo CCM, ACT, DP, CUF, NLD, CHAUMA, NCCR na CCK,
Gauday amesema kuwa zoezi la uchukuaji fomu limefanyika vizuri huku wagombea wote wamerudisha,ambapo mwisho wa zoezi la uchukuaji fomu na kuteua wagombea mwisho ilikuwa Agosti 28 ,mwaka huu kwa Mkoa mzima wa Mbeya.
Shaban Mwanjali ni mgombea Udiwani Kata ya Rujewa kupitia chama cha DP,amesema toka kuanza zoezi hilo hakuna changamoto yeyote iliyojitokeza.

More Stories
TAMWA yakumbusha jamii kupinga ukatili wa kijinsia kuelekea siku ta wanawake Duniani
Wanawake washauriwa kuchangamkia fursa za uchumi
Aida:Wanawake wakipata haki zote itapunguza migogoro